June 18, 2008

Karibu Bongo Kelly Rowland

Bila shaka utakuwa bado unalikumbuka kundi maarufu la muziki lililokuwa linajulikana kama Destiny’s Child kutoka nchini Marekani. Miongoni mwa mabinti waliokuwa wanaunda kundi hilo ni Kelly Rowland(pichani).Wenzake walikuwa ni Beyonce Knowles(mke wa Jay Z hivi sasa) na Michelle Williams. Kundi hilo lilivunjika rasmi mwaka 2005 ingawa mara moja moja bado huwa inatokea wakafanya maonyesho pamoja. Baada ya kuvunjika kwa kundi lao na kila mmoja kuendelea kivyake na shughuli za kimuziki,uigizaji nk, Kelly Rowland amekuwa akijitolea sana kwa huduma za kijamii.Hali hiyo ndio imemfanya achaguliwe hivi karibuni kuwa Balozi wa Taasisi ya MTV Staying Alive ambayo imejikita katika kupigana vita na maradhi ya ukimwi pamoja na matokeo yake kama vile kuwanyanyapaa walioathirika nk. Ni katika wadhifa huo wa “ubalozi” ambapo Kelly Rowland anatarajiwa kutua nchini Tanzania hivi leo ikiwa ni katika ziara yake katika nchi kadhaa za Afrika ikiwa na nia ya kueneza ujumbe na kuendeleza kazi za taasisi hiyo. Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania ambao ndio wenyeji wake,Kelly Rowland anatarajia kutembelea vituo kadhaa vinavyojishughulisha na mapambano dhidi ya ukimwi na pia kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara yake. Akimaliza ziara yake nchini Tanzania,Kelly Rowland anatarajiwa kuelekea Kenya na kisha Ghana,Msumbiji na Angola. Halafu bonyeza hapa uone jinsi mwanamuziki huyu na nduguze walivyopewa heka heka na nyani katika mojawapo ya nchi za kiafrika anazozitembelea. By BC.
Posted by Picasa

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...