April 15, 2008

Sura za Bongo or Face of Tanzania

Kampuni ya kitanzania ya Beatiful Tanzania Agency inayojihusisha na mambo ya urembo hapo jana imewataja washiriki watano bora kutoka katika shindano linalojulikana kama Face of Tanzania, ambao watakwenda nchini Afrika Kusini hapo kesho kwa ajili ya kupata uzoefu mbalimbali katika fani hiyo. Kampuni hiyo ipo chini ya usimamizi wa warembo maarufu wa kitanzania, Irene Kiwia na Nancy Sumary.
Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo kwa vyombo vya habari, warembo hao watano ambao wametajwa kuwa ni Edna Makanzo,Emmy Malau,Irene Shirima,Neshino Laizer na Yvone Joseph. Warembo hao ni miongoni mwa warembo 16 walioanza shindano hilo kabla ya kuchujwa na kubakia warembo 10 na hatimaye 5 hivi sasa ambao ndio wanaelekea Afrika Kusini kwa uzoefu zaidi.
Warembo hao ndio wanaotarajiwa kushiriki katika fainali tarehe 26 Aprili katika ukumbi wa Ubungo Plaza. Wakiwa nchini Afrika Kusini, washiriki hao wanatarajiwa kutembelea makampuni kadhaa ya uwakala wa urembo kama vile O-Model Afrika na pia kufanya mazungumzo mbalimbali na warembo wa kitanzania wafanyao shughuli zao huko kama vile Happiness Magessa na wengineo ili kujua zaidi undani wa shughuli hizo.
Pichani juu ni warembo hao watano wakiwa na maboss wao Irene Kiwia(mbele kulia) na Nancy Sumary(kushoto) wakati wa utangazwaji wa majina ya warembo hao katika hoteli ya Regency Mikocheni jijini Dar hivi leo. Warembo hao waliosimama kutoka kushoto ni Edna Makanzo,Emmy Malau,Irene Shirima,Neshino Laizer na Yvone Joseph.Mikononi wameshikilia pasi zao za kusafiria

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...