August 2, 2012

Hongera Assah Mwambene.

Hongera Asah A. Mwambene (41) kwa kuteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), hii ni nafasi kubwa na muhimu kwa taifa letu na zaidi katika tasnia ya habari. 

Mh Rais Jakaya Kikwete ameakuamini sana hata kukuteua kuongoza idara hii nyeti katika kipindi zama hizi za taarifa ama Information Age ktk karne hii ya mawasiliano ya Sayansi na Teknologia, bila shaka unazo sifa na weledi kuongoza idara hii, japo ina changamoto nyingi, sote wanahabari twajua, tumia weledi, elimu, maarifa na zaidi busara katika si tu kuongoza bali pia kuibadili iendane na wakati tuliomo. 

Hizi ni Zama za Taarifa na sote twajua "Information is Power", ushauri wangu ni mdogo sana, ifanye idara hii iendene na wakati, najua umesafiri sana nje ya nchi na kupata nafasi ya kujionea jinsi idara kama hizi katika nchi za wenzetu zinavyofanya kazi, kisasa zaidi, kitaaluma zaidi, na kiufanisi zaidi, zaidi ya yote kwa muda muafaka, kwani uzito wa habari ni muda. 

Nafasi yako sasa ni ya kiutawala zaidi, si vibaya ukawa mwanafunzi wa gwiji wa mambo ya utawala, John Maxwell, ameandika na kuotoa vitabu na machapisho mengi sana juu ya LEADERSHIP, pata nakala kadhaa, sina shaka zitakufanya kuwa mtawala bora, kila la kheri katika wadhifa wako mpya.

Rwebangira Blog. 
 

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...