Wakati huu ambapo visiwa vya Zanzibar vingali katika simanzi
kuu huku hakuna idadi rasmi ya watu waliokufa na kuzikwa ama (300, 1696 au
2000!) katika meli Mv Spice
Islanders 1 baharini, (kama ilivyokuwa kwa Mv Bukoba 1996) na ambapo mapaka
sasa nahodha hajulikani alipo ikiwa ni miongoni mwa waliokufa au la, angalau
Mmiliki au wamiliki wamejitokeza na kutangaza kulipa fidia.
Mmiliki huyo ni Visiwani Shipping Cooperation, kampuni
inayomilikiwa na:
- Salum Said Mohamed (Batashi) hisa asilimia 73 (Mkurugenzi)
- Makame Hasnuu Makame 15,
- Yussuf Issa Suleiman 12,
Kwenye mitandao, hasa wikipedia mmiliki pekee anayeonekana ni Makame Hasnuu na si Visiwani Shipping Cooperation.
Read more:
Read more:
Abiria waliokufa na wale waliosalimika katika ajali ya ya Spice Islander I watalipwa fidia na Kampuni iliyokuwa ikimiliki meli hiyo ya Visiwani Shipping Cooperation ya mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Salum Said Mohammed (Batashi), amesema fidia hiyo itatatokana na malipo ya bima kati ya kampuni hiyo na Shirika la Bima la Alliance Insurance ya jijini Dar es Salaam.
Alisema kampuni yake ilikata bima ya abiria yenye thamani ya Dola za Marekani 300,000, lakini alisema watu watakaonufaika na bima hiyo ni wale tu ambao wameathirika katika tukio hilo, “Abiria watalipwa bima walioathirika na wale ambao wamepoteza ndugu zao watanufaika kwa niaba yao,” alisema.
Hata hivyo, alisema watu waliopoteza mizigo hawatalipwa fidia kwa sababu sheria za kimataifa bima ya mzigo inayosafirishwa kwa meli hutakiwa kukatwa na muhusika wa mzigo huo.
Alisema meli hiyo ilikuwa imekatiwa bima na Kampuni iliyokuwa ikimiliki ndiyo itakayonufaika na bima hiyo, lakini hakutaja ilikuwa imekatiwa kiwango gani cha bima meli hiyo.
Alisemameli iliyozama ina umri wa miaka 37 tangu ilipotengenezwa kiwandani mwaka 1974 nchini Salamis- Ugiriki na kampuni ya Goumas Shipyard. Aidha, alisema meli hiyo ilisajiliwa Zanzibar Oktoba 10, 2007 na ilikuwa ikitoa huduma kati ya visiwa vya Unguja, Pemba na Tanzania Bara. Alisema kwa mara ya mwisho meli hiyo imefanyiwa ukaguzi na Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA) Disemba, 2010 na ilipelekwa Chelezoni Mombasa Julai 20 hadi Agosti 8, mwaka jana na matengenezo yote yalifanywana Kampuni ya Africa Marine ya Mombasa, “Ripoti baada ya kutoka Chelezoni Mombasa inaonyesha meli ilikuwa na uwezo wa kuendelea na kazi kama kawaida na haikuwa na matatizo yoyote,” alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema meli hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchukua tani 425 za mizigo na abiria 600 na wakati ajali hiyo inatokea ilikuwa na mzigo wa tani 97 na abiria 610.
No comments:
Post a Comment