September 18, 2011


Rais wa SMZ ametemelea visiwa vya Pemba na kuwa pole wakazi wa Visiwa hivyo kutokana na mkasa wa ajali ya meli ya Mv Spice Islanders 1 ambapo watu wapatao 200 wamepoteza maisha, 612 kuokolewa huku mamia wengine hawajulikani walipo.Dr Shein aunda Tume kuchunguza ajali Mv Spice Islanders 1
Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla walipokea kwa masikitiko, huzuni na majonzi makubwa taarifa ya kuzama kwa Meli ya MV.Spice Islander katika Bahari ya Hindi karibu na Nungwi usiku wa kuamkia tarehe 10 Septemba 2011 ambapo watu 612 waliokolewa wakiwa hai na maiti 203 zimepatikana mpaka sasa. Ili kujua ukweli kuhusu chanzo cha ajali hiyo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kuunda Tume ya kuchunguza ajali hiyo.
 
 
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee inaeleza kwamba kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Sheria ya Tume za Uchunguzi Sura ya 33 ya Sheria za Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein ameunda Tume ya Kuchunguza Ajali ya Kuzama kwa Meli ya MV. Spice Islander ambayo itakuwa na Mwenyekiti, Wajumbe na Katibu kama ifuatavyo :-
 
 
 
  1. Mhe. Jaji Abdulhakim Ameir Issa – Mwenyekiti
  2. Meja Jenerali S.S Omari – Mjumbe
  3. COMDR. Hassan Mussa Mzee – Mjumbe
  4. Capt. Abdulla Yussuf Jumbe – Mjumbe
  5. Capt. Abdulla Juma Abdulla – Mjumbe
  6. Bw. Salum Toufiq Ali – Mjumbe
  7. Capt. Hatib Katandula – Mjumbe
  8. Bi. Mkakili Fauster Ngowi – Mjumbe
  9. Bw. Ali Omar Chengo – Mjumbe
  10. Bw. Shaaban Ramadhan Abdulla - KatibuMwenyekiti wa Tume hiyo , Mhe. Jaji Abdulhakim Ameir Issa ni Mwanasheria mzoefu ambae kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
 
 
 
Meja Jenerali S. S. Omari ni Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), COMDR. Hassan Mussa Mzee ni Mkuu wa Kikosi cha KMKM na Capt. Abdulla Yussuf Jumbe ni Nahodha mzoefu wa meli za kitaifa na meli za Kimataifa, ambapo pia aliwahi kuwa nahodha wa Meli ya MV. Mapinduzi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
 
 
Capt. Abdulla Juma Abdulla, alikuwa katika Kikosi cha KMKM kwa muda mrefu ambapo sasa ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Idara Maalum za SMZ na Bw. Salum Toufiq Ali ni Mwanasheria wa siku nyingi Zanzibar ambae ana uzoefu wa sheria za bahari, ambae kwa sasa ni Mwanasheria wa kampuni ya ZANTEL
 
 
.
 
Capt. Hatibu Katandula ni Mkufunzi katika chuo cha Ubaharia cha Dar es Salaam na Bi Mkakili Fauster Ngowi ni Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Tanzania.
 
 
 
Bw. Ali Omar Chengo aliwahi kuwa mwanajeshi katika JWTZ na baadae kufanya kazi kwa muda mrefu katika Kikosi cha KMKM kabla ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na Naibu waziri wa Mawasiliano katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar huko nyuma.
 
 
 
Katibu wa Tume hiyo Bw. Shaaban Ramadhan Abdulla ni mtaalamu wa Sheria za bahari, ambapo kwa sasa ni Mwanasheria katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP).

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...