September 15, 2011

News Alert, Mv Spice Islanders 1 - Wasauzi wasitisha zoezi la uokoajiVikosi vya uokoaji toka Afrika kusini vyasitisha zoezi la kuopoa miili iliyobaki baada ya kushindwa kuifikia meli kutokana na hali ya bahari na umbali ilipo meli.   Uwezo wao wa kupiga mbizi ni mita 54 tu lakini Mv Spice Islanders 1 inasemekana iko umbali wa zaidi ya nusu kilomita. Wanasema wataagiza meli maalumu yenye uwezo wa kufika umbali huo.
Source: TBC

My take,
Mosi. toka siku ya kwanza ilisemekana kuwa meli imezama umbali usiopungua mita 300, hivyo wakati wakijiaanda kuja walishajua kuwa kuna umbali huo, naamini kuwa hilo walilijua, kwanini hawakujiandaa kiasi hiko?

Pili. Walipofika tulitaarifiwa kuwa wamekuja na vifaa maalum vya kisasa kwa zoezi husika, sasa wanaposema kuwa inabidi waagize meli nyingine yenye uwezo mkubwa zaidi wanamaanisha nini?

Tatu. Ikiwa waliyajua yote hayo na wao wakijua kuwa uwezo wao wa kupiga mbizi ni mita 54 tu kwanini bado walijiaanda, wakafunga safari na hatimaye kwenda kuzuga tu baharini? ndio ni kuzuga, kwa sababu ikiwa unajua hautoweza kufanya kazi husika unapojifanya waenda kuifanya wakuwa wafanya nini?

Hii si habari njema kipindi hiki ambapo twaambiwa kuwa watu wapatao 2000 bado miili yao haijapatikana, je ndugu wa hao 2000 watawaonaje hawa? watalii au?

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...