Pengine ni ndoto za mchana au ni jinamizi lilinikumba nikajikuta naota eti Mahakama ya Rufaa imeuzwa na ati inatarajiwa kuvunjwa, siamini, nadhani ni ndoto za mchana tu ndo zinanisumbua, sidhani kuwa serikali yangu hii, niloichagua na kuiweka madarakani inaweza kufanya jambo kama hilo, sidhani, na haiwezekani.
Ndoto za mchana uwa ni mbaya wakati mwingine, ni rahisi kuota umeokota bulungutu na kuamka ukiwa lofa zaidi, eti ile hoteli jirani yake imeihisi inabanwa na mahakama ile na sasa inataka iondoe kiwingu, ati wageni wakiona majoho ya waheshimiwa majaji wetu wanaweweseka vyumbani, mvinyo haupandi, wanaota majinamizi! Mhh ni kweli habari hii? Mbona yule kiongozi wa taifa kubwa kabisa duniani alilala hapo siku kadhaa na hakuweweseka? ahh, ndo mambo ya ndoto hayo unakurupuka unadhani ni kweli, walinganisha na uhalisia waona kuna walakini ndo wagundua, kumbe ni ndoto tu.
Lakini mbona ndoto hii imekuwa ndefu hivi? ati kuna wataalamu fulani (si wa sheria) wanataka kuandamana kupinga kuvunjwa kwa mahakama hii? mhh yawezekana bado niko ndotoni, hivi wanasheria si ndo wangekuwa wakwanza kuandamana? sasa iweje wale, wanaitwaje vileee?? enhee, wasanifu ndo wawe na kimbelembele kuandamana??? Si mwaona mambo ya ndoto hayo, lakini kama ingekuwa ni kweli hata mimi ningewaunga mkono, ningeandamana, sijui mpaka wapi, kokote kule.
Ahh! ndo mambo ya ndoto za mchana hayo, usiombe ukaota, zinadanganya sana, hebu we fikiria serikali makini kama hii kweli yaweza kufanya uamuzi wa kijinga kama huo? hata siku moja haiwezekani, ni ndoto hizo, tena za mchana, silali tena mchana nisije jikuta naota na Ikulu nayo imeuzwa bure!
Jamani puuzieni, ni ndoto tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH

The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA Agosti16, 2008 PRESS RELEASE Mkuu wa Chuo cha Kijeshi (TMA), Monduli Arusha, Brigedia Jenerali...
-
Wastaafu Rais Mkapa na Lowassa wwalipokutana ktk msiba wa Mzee Bhoke Munanka.
-
WINNERS Boulevard.: Biashara ya Masoko ya Mtandao : Fikiria kama ungekuwa walipwa kwa kila ushauri wa kutumia huduma ama bidhaa ya kampuni a...
-
Mechi kati ya Watani wa jadi ndo imemalizika huko mji kasoro bahari kwa Yanga kuendeleza uteja kwa kulala gori moja bila. Juzi tu vijana ha...
-
President Dr Jakaya Mrisho kikwete with NASDAQ's Vice Chairman David Wicks (right) and at the MarketSite at New York 4 Times Square ...
-
But while the suspect was being attended to in one of the wards at Leratong Hospital in Krugersdorp, west of Johannesburg, the on-...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
Gadhafi na Obama With reported pockets of fighting remaining in Tripoli on Wednesday, the whereabouts of Lib...
1 comment:
Tanzania kila kitu kinawezekana, ukweli ama ndoto, vyote vinawezekana tu.
Post a Comment