Kuna mambo mengine huwa hayaiingii akilini haraka hasa kwa watu wenye akili za kawaida kama za kwetu, sielewi uamuzi ule uliosabibisha usumbufu usio na sababu yoyote nchini mwetu ulikuwa na maana gani au manufaa gani kwa mtu mmoja mmoja ama taifa, sielewi.
Kwa vipimo vyovyote vile manufaaa ya uamuzi ule ni madogo kuliko madhara yake, kwanini? mara baada ya uamuzi wa kushusha bei ya mafuta (kwa vigezo vyovyote vilivyotumika, ama vya kisiasa) tulishuhudia mambo ambayo hatukuwai kushuudia katika sekta hii, vituo viligoma kuuza, makampuni ya mafuta yakagoma kupeleka mafuta vitioni, kiongozi wao akatoa sharti la masaa 24 (kwa kimombo - ultimatum) iongeze bei ama sivyo...., matokeo yake ni kukosekana kwa mafuta katika sehemu kubwa ya nchi na pale yalipopatikana yaliuzwa kwa bei ya kuruka, kuna taarifa kuwa baadhi ya sehemu ilifika Sh 5,000 kwa lita moja na mpaka sasa haijatengemaa.
leo hii wiki moja tu baada ya kasheshe yooote hiyo tunaambiwa yamepanda tena, sababu pesa yetu ya "madafu", huku bado hata machungu ya uamuzi wa mwazo hayajaisha, baadhi ya mikoa mpaka sasa bado haijapata mafuta, aliyepewa adhabu wala hajaanza kui-feel, na hali ya mafuta haijatengemaaa, twaambiwa ni kushuka kwa thamani ya shilingi! mtu atajiuliza, lini shilingi yetu iliwai kupanda???, je kulikuwa na sababu gani kushusha bei na kuleta usumbufu huu?? je si ni rahisi mtu kuunganisha moja na moja ukapata mbili? kwamba haya ni matokeo ya ile ultimatum ya mabwanyenye wa mafuta????
Tutafakali!!
No comments:
Post a Comment