March 9, 2011

Murigariga, Loliondo, Mch Mwasapile, Serikali na Magazeti

Umati unazidi kumiminika kwa Mch Mstaafu Ambekile Mwasapile (Babu) kupata kikombe cha "UZIMA" toka mmea unaojulikana kama "Murigariga".
Babu anasema alioteshwa kuwa mti huo wa porini na Mungu na kuwa unatibu magoniwa yote sugu, sharti ni kuwa ni lazima yeye ndo akupe kikombe hicho cha "uzima" ndo unapona, ukienda kujitengezea mwenyewe haifanyi kazi, bila shaka ndo sababu ya umati mkubwa kujazana katika kijiji kidogo cha Samunge huko Loliondo.
Taarifa mbali mbali toka magazetini zasemaje?/
Mwananchi:-
Vigogo wasababisha vurugu Loliondo.
WATU wanaodaiwa kuwa ni vigogo wa Serikali wamesababisha vurugu kubwa katika Kijiji cha Samunge, Tarafa Sale, Loliondo kunakotolewa tiba ya magonjwa ya sugu na Mchungaji Mstaafu, Ambilikile Mwasapile baada ya kuvuruga utaratibu wa foleni kabla ya kupata huduma hiyo.Vurugu hizo zilianza pale kundi la watu lilipobaini kuwa vyombo vya dola, askari polisi na wanamgambo waliokuwa wanalinda usalama katika eneo hilo, wanawasaidia vigogo kuwahi kunywa dawa kwa kukwepa foleni. Hali hiyo ilisababisha wananchi kupoteza imani na ulinzi huo na kuamua kuziba barabara zilizokuwa zinakwepa foleni kwa kutumia mawe na magogo. Hata hivyo, vigogo hao waliamua kuacha magari yao na kuanza kuelekea nyumbani kwa Mchungaji huyo kwa miguu kitendo ambacho kiliwafanya wananchi kuamua kuvamia jiko linalotumika kutengeneza dawa hiyo na kuanza kuinywa bila mpangilio jambo lililosababisha utaratibu wa kutoa dawa kusitishwa kwa saa saba.
Nipashe:-
Dawa ya Mwaisapile inaponya.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limesema linatambua na kubariki dawa inayotolewa na Mchungaji wake mstaafu anayefanyia shughuli zake Loliondo, Ambilikile Mwasapile, huku baadhi ya maaskofu wa kanisa hilo wakithibitisha kwamba wamekunywa dawa hiyo na kuponywa.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kwa njia ya simu, Maaskofu wa kanisa hilo Thomas Laizer wa Dayosisi ya Mkoani Arusha, Dk. Martin Shao wa Dayosisi ya Kaskazini, walisema huduma inayotolewa na Mchungaji Mwasapile ni sahihi na imeanza siku nyingi na kwamba wao ni miongoni mwa watu wa mwanzoni waliowahi kunywa dawa hiyo na kupona.

Askafu Laizer alisema kwa mujibu wa imani na taratibu za KKKT, mchungaji huyo yupo sahihi na Kanisa halina mgogoro naye.

Habari Leo:-

Serikali yatoa usafiri kwa Mganga wa Loliondo.

SERIKALI imeanza kusaidia huduma mbalimbali kwa wananchi waliomiminika kijijini Samunge, Tarafa ya Sale, Loliondo wilayani Ngorongoro, kwa tabibu Ambilikile Masapila, kupata kile kinachoaminika kuwa ni tiba dhidi ya magonjwa sugu, kwa kumpatia vifaa likiwemo gari la kubebea dawa, vikombe na sufuria.
Aidha, Serikali imeanza kujenga vyoo vya muda katika maeneo waliojazana watu huku misururu hiyo ikizidi kuongezeka na kufika katika misitu jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya watu hao.
Akizungumza na HabariLEO kwa simu jana jioni, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, Elias Wawa Lali alisema ametembelea katika eneo hilo jana mchana na kuacha misururu ikienda kwa kasi kutokana na mchungaji huyo kupatiwa baadhi ya vifaa na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Tanzania Daima:-
Mchungaji wa Loliondo awa mbogo.

MCHUNGAJI mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambukile Mwasapile (78), wa kijiji cha Samunge-Loliondo, wilayani Ngorongoro, Arusha amewashukia walanguzi wanaotoza nauli na kuuza bidhaa kwa bei kubwa kwa wagonjwa wanaoenda kupata huduma kwake, kwamba watafilisika.

Walanguzi hao ni pamoja na wale waliopandisha bei ya nauli za usafirishaji kutoka maeneo mbalimbali nchini, wanaosafiri kuelekea kijijini hapo kupata tiba za mchungaji huyo za kimiujiza, wauzaji wa vyakula na vinywaji wanaouzia wagonjwa wanaopata tiba kwa mchungaji huyo.

Maji aina ya Kilamanjaro ya lita moja na nusu katika mji wa Arusha, yameadimika baada ya wafanyabiashra kuyachukua na kuyapeleka katika kijiji hicho ambako yanauzwa kwa bei ya kati ya sh 2500 na 3000.

Nauli za usafirishaji wa abiria kwa mfano kutoka Arusha zimepanda toka shilingi 35,000 na 50,000 hadi 120,000 na 180,000 kutegemeana na aina ya usafiri huku bei za bidhaa mbalimbali kama maji na vyakula zikipanda maradufu katika kijiji hicho ambacho huduma hiyo inatolewa.

The Citizen:-

Loliondo death toll reaches six.

Arusha. The rush to Loliondo for a miracle cure from a spiritual healer is slowly turning into a humanitarian crisis after four more people were reported to have died while queuing to reach the ‘doctor’.This brings to six the number of people reported so far to have lost lives while queuing to see the medicine man who claims to have divine powers to heal.
Commenting on the deaths yesterday, the Ngorongoro district commissioner, Mr Elias Wawa Lali, said most of those who died may have been rushed there directly from their hospital beds while in critical condition.However, he said one of the reported deaths was that of a child crushed by one of vehicles that have ferried hundreds of people to the area.
“The child was sleeping under a vehicle while the parents had gone to consult the miracle healer,” he told The Citizen on the phone from Samunge village. Mr Wawa Lali could not give the names of the deceased or where they had hailed from. One of them was, however, said to have come from Manyara Region.
“The problem we are having is that some of the patients taken there for treatment were moved out of hospital while in critical condition,” he said. The district administrator pleaded to those intending to take their relatives there to avoid picking critically ill people from hospital beds.On Monday night the DC confirmed two people had died while waiting to reach the healer whose miracle cure has led to an influx of patients to the remote village.
BBC Swahili>
Mganga wa Loliondo azua sokomoko.
Mchungaji mmoja mstaafu wa Arusha kaskazini mwa Tanzania anayedai kutibu magonjwa sugu, amevuta umati wa watu wanaokwenda nyumbani kwake kupata tiba hiyo. Hivi sasa imedhihirika kuwepo maelfu ya watu wanaosaka tiba na wengine kuwapeleka jamaa zao wanaosumbuliwa na maradhi yasiyotibika, kiasi cha jeshi la polisi kupeleka askari kuimarisha ulinzi kwa mchungaji huyo. Tayari wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeanza uchunguzi kuhusu tiba inayotolewa na mchungaji huyo. Mwandishi wetu Ben Mwang’onda anaarifu.
Mtanzania.
Dawa ya UKIMWI yatikisa

WAKATI maelfu ya watu wakiendelea kumiminika katika Kijiji cha Samunge wilayani Ngorongoro kupata kile wanachoamini kuwa ni tiba ya maradhi makuu matano, ukiwamo Ukimwi, baadhi ya hospitali katika mikoa ya Arusha na Manyara imepungukiwa wagonjwa.

Uchunguzi uliofanywa na timu ya MTANZANIA umebaini kuwa baadhi ya wagonjwa, ama wameondoka wenyewe hospitalini, au wametolewa na ndugu zao na kupelekwa Samunge kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila.

Foleni ya magari imeelezwa kwamba sasa imefikia kilomita 20 kutoka kijijini, hali iliyoilazimu Serikali iingilie kati kuzuia magari yasizidi kwenda huko hadi waliopo watakapokuwa wamepata dawa (kikombe).

Wingi wa watu na ukosefu wa miundombinu ya kujisaidia ni tishio jingine la mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza.

Mwasapile anatoa dawa kwa wagonjwa wa Ukimwi, kisukari, pumu, saratani, shinikizo la damu na mengine kwa “sadaka” ya Sh 500 tu. Masharti ni kwamba lazima mgonjwa anywe dawa hapo hapo nyumbani kwake. Dozi ni kikombe kimoja tu.

2 comments:

Anonymous said...

Wizara ya afya inapoteza muda kucgunguza dawa hiyo kitaalamu. Huyop mchungaji alioteshwa, hakutumia sayansi yoyote. Hiyo dawa ni kitu cha muujiza, sidhani wizara ya afya ina uwezo wa kupima miujiza!!

Photography Tips said...

The photos look great. Great information and article. Thanks for sharing.

Google+ Followers

There was an error in this gadget
There was an error in this gadget

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...