Baada ya CCM kumteua Dr Ali Mohamed Shein kuwa mgombea urais kwa upande wa Zanzibar na pengine kukaribia kuweka historia mpya kwa Visiwa hivyo kutawaliwa na mtu toka Pemba, kitendawili kingine na PENGINE historia mpya uenda ikawekwa muda si mrefu pale atakapotangazwa mgombea mwenza wa Rais Jakaya Kikwete.
Inabashiriwa na wachambuzi wa mambo na siasa za Bongo pamoja na mwelekeo na utawala wa JK kuwa uenda kwa mara ya kwanza akamteua mwanamke kuwa Mgombea mwenza na hivyo kupelekea kuwa na Makamu wa Rais wa kwanza mwanamke.
Je ikiwa hivyo ndivyo, ni nani basi mwanamama huyo??
No comments:
Post a Comment