DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425 | | PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la Mawaziri leo, Ijumaa, Machi 12, 2010, katika kikao chake kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam, chini ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limejadili hali ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na kufanya maamuzi ya msingi kwa kukubaliana kama ifuatavyo:
· Kwamba Serikali ianze mara moja kujadiliana na RITES, mbia wa Serikali katika kampuni ya TRL, kwa lengo la Serikali kununua hisa 51 za RITES katika kampuni hiyo. Kwa sasa RITES inamiliki asilimia 51 na Serikali inamiliki asilimia 49 katika TRL.
· Kwamba baada ya hapo, Serikali itafanya matayarisho ya msingi ikiwa ni pamoja na kurekebisha kasoro na kuangalia mustakabali wa TRL, na kuiandaa kampuni hiyo kwa ajili ya kutafutiwa mbia mwingine wa kushirikiana na Serikali katika kuendesha TRL.
(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU WA BARAZA LA MAWAZIRI
OFISI YA RAIS,
IKULU.
12 Machi, 2010
No comments:
Post a Comment