Chama cha wapiga picha za Habari nchini Press Photographers Association of Tanzania (PPAT) leo hii kimezaliwa upya ama kufufuka rasmi baada ya kukaa domant kwa takribani miaka kadhaa na kufanya mkutano mkuu na kufanya uchaguzi kwa viongozi, ambapo viongozi wa zamani waliamua kujiuzulu na kupisha kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wapya.
Katika uchaguzi huo Mwanzo Millinga aliibuka kuwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti, John Badi Mwenyekiti Msaidizi, Katibu Mkuu ni Mroki Mroki akisaidiwa na James Mpangala nafasi ya Mwekahazina ilienda kwa Leah Samike ambapo atasaidiwa na Mwanakombo Jumaa.
Wajumbe wa Kamati ya utendaji ni Khalfan Said, Moshi Kiyungi, Mpoki Bukuku na Ramadhani Tonge.
No comments:
Post a Comment