Wadau Tumsaidie Mtoto Tuntufye..
MZAZI wa mtoto Tumtufye Mwakasaka (8) ambaye kwa sasa amekatisha shule kuja mkoani Iringa kutafuta wasamaria wema kwa ajili ya kunusuru maisha yake baada ya mwili wake kuvimba mithiri ya pipa wamemwomba Rais Jakaya Kikwete pamoja na wadau wote kusaidia kunusuru uhai wa mtoto huyo.
Mtoto huyo ambaye anahitaji msaada wa fedha zaidi ya shilingi milioni 5 kwa ajili ya kwenda nchini India kutibiwa kwa sasa anaishi katika eneo la Bwawani kihesa kilolo katika Manispaa ya Iringa huku akiendelea kutabika baada ya mwili wake kutokwa na malenge lenge sehemu za siri na maeneo mengine huku akiendelea kuvimba mwili kutokana na maradhi ya figo yanayomsumbua.
zaidi mtembelee Fransis Godwin
No comments:
Post a Comment