Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Profesa John Mkoma, alisema wamelazimika kuongeza muda huo kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa usajili ikiwamo tatizo la umeme vijijini.
“Kutokana na tathmini iliyofanyika na kwa kuzingatia maslahi ya watumiaji pamoja na watoa huduma, TCRA imeongeza muda wa kusajili namba za simu kwa muda wa miezi sita mingine hadi Juni 30, mwakani,” alisema Profesa Mkoma.
Alisema pamoja na kwamba tangu usajili huo uanze Julai mosi, mwaka huu hadi Desemba 20, watumiaji milioni 6.3 ambao ni sawa na asilimia 43 wameshajisajili na kuingizwa kwenye data, lakini utaratibu huo umekuwa ukikabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zimekwaza usajili huo hasa vijijini.
TCRA iliamua kuanzisha utaratibu wa kusajili namba za simu Mwaka huu ili kulinda watumiaji na matumizi mabaya ya huduma hiyo ya mawasiliano , kuwezesha kutambua watumiaji wa huduma za ziada za simu kama huduma za kibenki nakadhalika, kuimarisha usalama wa taifa na kuwawezesha watoa huduma kufahamu wateja wao na kuwahudumia.
No comments:
Post a Comment