August 4, 2009

Marupurupu ya kamera

Kitchen pati ya Sarah, Kapendeza kweli jamani
Kila kazi ina marupurupu yake lakini ya kamera yamezidi, siku mmoja kabla ya kuja huku sauzi nilipewa kazi na rafiki yangu mpendwa kumtaswiria ka sherehe ka jikoni ka mchumba au mke mtarajiwa wake, sikukumbuki lini mara ya mwisho kufanya kazi ka hii, pengine miaka kadhaa imepita sasa,
Niliwai kusema wakati fulani kazi ya picha ina marupurupu au nafasi kubwa ya kuijichjanganya na kila makundi ktk jamii na bado ukaonekana ni mmoja wao, yaani yaweza tokea asubui ukapata chai na wafanyabiashara wakubwa au "mataikuni" na ukasikia wakijisiu kwa kufanikiwa kwao ama wakipnga mikakati ya kuingiza mabilioni mengine kadhaa na mchana wa siku hiyo ukajikuta wapiga miayo na watoto wa mitaani wakieleza maswaibu yao au wamachinga na mgambo wa jiji wakitunishiana misuli na jioni yake ukajikuta katikati ya mashabiki wa mpira wakipena tambo zao za Simba na Yanga na pengine ukiwa na baati mbaya likatokea jambo ukijikuta waambulia mabomu ya machzo.
Lakini kabla siku haijaisha waweza kujikuta huko katika pati kama hizi za jikoni, "mikia ya jogoo" ama Cocktail za mashirika kadhaa au zaidi ukajikuta huko Ikulu pamoja na marais na viongozi wa nchi katika moja ya dhifa za Kitaifa, naamu hayo ndo marupurupu ya kazi hii.
Hivi inakuwaje unapojikuta katikati ya kundi la kinadada wapatao mia na ushee katika shereha ya jikoni iliyosheeni kinywaji cha aina ya mvinyo?? Kisia Mdau kwa leo CIAO

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...