June 29, 2009

Familia iliyoteketea kwa Moto Dar yaagwa,

Vifo hivi kwa Familia ya Grayson Naftari vyatufunza nini wakazi wa jiji?
Baadhi ya waombolezaji wakipita kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu watano wa familia moja waliokufa kwa ajali ya moto mwishoni mwa wiki jijini.
Mavyuma haya yaliyowekwa kwa nia njema ya kuzuia wezi na vibaka kuingia ndani kiurahisi na kukwapua mali za wenye nyumba (na ukizingatia Manzese ilivyomaarufu kwa vibaka) lakini vimekuwa pia ni kikwazo kwa wasamalia wema na majirani kuingia na kuwaokoa wakti wa moto huo ulipozuka na pia vikawa ni kikwazo hata kwa wao wenyewe kuweza kujiokoa hata kujikuta wakifa huku wakijiona. MUNGU WALAZA MAHALA PEMA PEPONI. AMEN!
Watu watano wa familia moja, akiwamo mtoto wa mwaka mmoja, wamekufa kwa kuteketea na moto uliozuka ghafla usiku wa kuamkia jana katika nyumba Manzese, Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, alisema moto huo ulizuka saa saba usiku katika nyumba ya mkazi wa Ndugumbi-Mpakani, Manzese, Grayson Naftali (64) na kuua watu wote watano waliokuwa wamelala ndani.
Alisema vyumba viwili kati ya vinne viliungua na mali zote za ndani pamoja na marehemu, akiwamo Naftali ambaye ni mstaafu wa Chama cha Wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL). Kamanda Kalunguyeye aliwataja wengine waliokuwamo ni Modesta Marapole (55) ambaye ni mke wa Naftali, msichana wa kazi aliyejulikana kwa jina moja Tabasamu (20), Clementiana Dawani (12) mwanafunzi wa darasa la sita wa shule ya Msingi Ndugumbi na mtoto wa mwaka mmoja, Lagano Richard.
Clementiana na Lagano ni wajukuu wa Naftali. Kwa mujibu wa Kamanda, chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme ambayo inasemekana ilianzia katika soketi ya televisheni na kusambaa katika vyumba na watu waliokuwa ndani kukutwa na mauti. Alisema moto huo ulizimwa na majirani na kikosi cha Zimamoto na watu waliokuwa ndani walikutwa tayari wameungua na kufa. zaidi soma habarileo

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...