February 2, 2009

"HIVI NDIVYO TULIVYOMUUA ALBINO"

SIMULIZI YA KUSIKITISAHA MUUAJI WA ALBINO SHINYANGA

Akisimulia tukio zima lilivyokuwa, Bw. Mawe alidai siku ya tukio akiwa na wenzake sita, walipanga kumuua Bw. Nkanyabilu kwa kushirikiana na shemeji yake, Bw. Sayi Gamani.

Alidai Bw. Gamani alimdanganya Bw. Nkanyabilu kuwa anampeleka hospitali kumtibu maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kabla ya kushirikiana kumkamata na kwenda kumuua. "Ilipofika saa saba usiku, tulimkamata Bw. Lyaku (Nkanyabilu) na kumpeleka mtoni, tulipofika huko tulimlazimisha kuingiza kichwa kwenye maji hadi alipokufa, tukamchinja, tukamkata miguu na baada ya hapo, tukaiingiza viungo hivyo kwenye gunia moja na mwili wake kwenye gunia lingine na kutumbukiza mwili wake kwenye maji," alidai. Alidai baada ya hapo, walibeba kichwa na miguu na walishauriana waviweke nyumbani kwake (kwa Bw. Mawe) wasubiri wateja hao ambao walikuwa wakiwasiliana nao kutoka Mwanza mjini, Lamadi na Kahama Mkuu wa Polisi wilayani Bariadi, Mrakibu wa Polisi, Bw. Paul Kasabago, akiwa eneo la tukio alisema kupatikana kwa viungo hivyo kumetokana na ushirikiano mkubwa wa wanakijiji hicho ambao aliwashukuru kwa kuonesha ushirikiano wa dhati na ulizi shirikishi. Aliwataja wanaoshukiwa na Polisi kuhusika katika tukio hilo kuwa ni Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Chenyenye Kishiwa (64), Bw. Sayi Gamanya (47), Bw. Gumbu Nzige (48), Bw. Mboji Mawe (48), Bw. Sayi Mafize (32) na Bw. Salum Mshamamba (52). Wote ni wakazi wa Mkingwabie.

1 comment:

Anonymous said...

Mheshimiwa mwenye blog hii, maelezo hayo hapo juu yanatia hasira na uchungu na ndio maana hata watu wazima tena wazito wanafikia hatua ya kumwaga machozi hadharani tena wakiwa kazini, mwee!!!... Yaani huyo jamaa anayeitwa Bw. Mawe anasimulia yeye mwenyewe walivyo-plan kumuua Bw. Nkanyabilu kwa kushirikiana na shemeji yake yaani huyo Bw. Sayi Gamani, hatimaye plan zao zilikamilika kwa kumuua, kumkatakata na kisha kuutosa mwili wa binadamu mwenzetu mtoni na yeye Bw Mawe kuondoka na viungo walivyovihitaji na kuvihifadhi nyumbani kwake, kisha amekamatwa tena na ushahidi kikiwepo kichwa cha marehemu Nkanyabilu kama ilivyoelezwa kwa kazi nzuri waliyoifanya wananchi!!!!... Sasa kinachonichanganya hapa na kuniudhi na nidhani ndicho kinawafanya na wengine kububujikwa machozi ni kwa nini polisi wanawaita huyo Bw. Mawe na Sayi Gamani kuwa ni WATUHUMIWA wakati wao wanasema ndio waliopanga na kutekeleza mauaji hayo???? jamani, mbona lugha hiyo haieleweki? inaudhi au mimi sielewi vizuri kiswahili? Kwangu mimi hao ni WAUAJI kwani wao wenyewe ndio wanasema walifanya kazi hiyo kwa mikono yao wenyewe, mwee nyie mkoje jamani!! nisaidieni. Mdau Ben Ben.

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...