WAFANYAKAZI wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) wameitaka Menejimenti ya Shirika hilo na bodi ya wakurugenzi kujiuzulu kwa kwa kile walichodai kushindwa kukabiliana na dosari zilizosababisha ndege za Shirika hilo kuzuiwa kuruka na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA).
Hatua hiyo imekuja siku moja tu baada ya Mkurugenzi wa ATC, David Mattaka kukiri kuwa shirika lake ilikaguliwa na kukutwa na dosari 482 ambazo zilipelekea TCAA kuiamuru kusimamisha huduma. Katika kikao cha dharura kilichoitishwa na chama cha wafanyakazi wa ATC (COTWU) jana Dar es Salaam, wafanyakazi hao walimtaka Mattaka na watendaji wenzake na Bodi kuachia ngazi.
“Hakuna sababu ya kulindana, wala kutafuta mchawi, mchawi wetu tuna mfahamu ni menejimenti na bodi yake, hawa wajiuzuru,” alisema mfanyakazi mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake.
“Menejiment imeshindwa kufanya mawasiliano na sisi kuhusu dosari hizo mpaka hali imefikia hapa … ukiachilia mbali wafanyakazi takribani 100 hawajalipwa mshahara wa Novemba,” alisema Mwingine.
No comments:
Post a Comment