Wh. Basil Mramba na Daniel Yona wataendelea kusota tena rumande hadi Jumatatu pamoja na mahakama kuu kuwalegezea masharti ya dhamana.
Mahakama kuu katika uamuzi wake wa jana, ililegeza sharti la kuwataka washitakiwa hao kutoa fedha taslimu, badala yake ikawapa mbadala wa kuwasilisha hati za mali yenye thamani ya Sh bilioni 2.9 kila mmoja.
Uamuzi wa kuwataka washitakiwa waweke fedha taslimu ulitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Hezron Mwankenja. Lakini sharti hilo lililegezwa jana na mahakama hiyo ya juu.
Uamuzi huo wa Jaji Njegafibile Mwaikugile licha ya ulipokewa kwa furaha na ndugu wa washitakiwa, haukuwasaidia sana kutokana na hati walizokuwa nazo kuonekana kuwa na dosari kadhaa ambazo zilihitaji uthibitisho kutoka kwa mamlaka zingine.
1 comment:
Ukisahau kuwa jela tokea zianzishwe kuna ambao wako jela miaka kibao bila makosa, unaweza kuwaonea huruma waheshimiwa vibaka.
Post a Comment