July 31, 2008

DEUS MALYA - ALIYEKUWA NA WANGWE

SEHEMU YA WARAKA WA CHADEMA KWA IGP MWEMA. Hivyo basi , Chadema kama Chama kilichoathirika kwa kumpoteza Mbunge wake, Mwenyekiti wake wa Mkoa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti na hivyo kuwa na maslahi ya karibu sana katika uchunguzi huu, tunalitaka Jeshi la Polisi wakishirikiana na vyombo vingine vya Usalama kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na mambo yafuatayo; 1. Kujua huyu ambaye alikuwa (Deus Mallya) na Marehemu kwenye gari lake wakati anafariki ni nani na anafanya shughuli gani. 2. Deus Mallya alienda Dodoma kufanya shughuli gani na ana uhusiano gani na Marehemu na au Familia ya Marehemu. 3. Ndugu Deus Mallya alikuwa amekaa kwenye kiti gani wakati ajali inatokea. 4. Ni nani alikuwa anaendesha Gari wakati ajali na hatimaye umauti unamkuta Mheshimiwa Chacha Wangwe. 5. Ni mazingira gani yaliyopelekea na au kusababisha ajali hiyo kutokea . 6. Tunataka Polisi wachukue hatua stahiki za kisheria ili Deus Mallya akaisaidie Polisi na kuhojiwa kwa kina juu ya suala hili kwani maelezo yake yana utata mkubwa sana. 7. Jeshi la polisi liitoe ripoti ya uchunguzi huo mapema na kuiweka ripoti hiyo hadharani. Tunapendekeza hatua hizo zichukuliwe mara moja kwani tunaamini kuwa kifo hiki kimeghubikwa na utata mkubwa sana na haswa kutokana na maelezo ambayo yamekuwa yakitolewa na aliyeshuhudia ajali (Deus Mallya) pamoja na watoto wa marehemu.
Posted by Picasa

No comments:

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...