September 8, 2011

Kumekucha Igunga

  • Pingamizi la CUF kwa CHADEMA na CCM Lakwama 
  • CHADEMA kuzindua kampeni leo
  • Polisi ya wafungulia jalada CHADEMA na CUF
  • Vyama vinane kuchua Igunga










CHAMA cha Wananchi (CUF), kimewawekea pingamizi wagombea ubunge kupitia vyama vya Chadema na CCM kwa madai kuwa hawakurudisha fomu kwa kufuata kanuni na sheria za uchaguzi. Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Msimamizi wa Uchaguzi, Magayane Protas alisema ametupilia mbali pingamizi hilo.“Mgombea wa CUF, Ndugu Mahona amewasilisha pingamizi dhidi ya wagombea wa Chadema na CCM akidai kuwa walirudisha fomu kinyume cha sheria. Lakini nimeangalia sheria inavyoeleza na kuona hawakufanya kosa lolote wakati wakirudisha fomu hivyo, nimelitupilia mbali pingamizi hilo.”

 Pia alisema mgombea wa SAU, John Magid aliwasilisha pingamizi dhidi ya wagombea wa Chadema na CCM akidai kuwa si wanachama halali wa vyama hivyo kwa kuwa ni wafanyakazi wa Serikali. Akizungumzia madai hayo, Magayane alisema Magid alisahau kuwa kuna waraka namba 1 mwaka 2000 ambao unaruhusu mtumishi wa umma kugombea katika chama.

 “Kwa bahati nzuri hawa wagombea wa Chadema na CCM walishaandika barua serikalini kuachia nafasi zao na barua zenyewe ni hizi hapa, hivyo ni halali wao kugombea,” alisema Magayane.

 Alisema kuwa kutokana na kujiridhisha, ametupilia mbali pingamizi hilo pia. Hata hivyo, Magayane alisema kuwa kama walalamikaji hawajaridhishwa na uamuzi wake, wanaweza kukata rufaa ndani ya saa 24.

 Alisema wagombea wa vyama vinane wamepitishwa kuwania ubunge wa jimbo hili ambao ni kutoka CCM, CUF, Chadema, Chausta, AFP, UPDP, SAU na DP.

 Chadema kuzindua kampeni leo
Chadema kinatarajia kuzindua kampeni zake rasmi leo. Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa chama hicho, Waitara Mwita alisema kuwa watawapokea viongozi wa kitaifa kwa maandamano kuanzia saa 6:00 mchana ili kuelekea kwenye eneo la mkutano katika Uwanja wa Sokoine.

 “Tutaanza maandamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa na wajumbe wa kamati kuu pamoja na wabunge na mkutano utaanza saa 8:00 mchana na kumalizika saa 12:00 jioni,” alisema

 Polisi yavifungulia mashtaka Chadema, CUF
Jeshi la Polisi limefungua jalada la mashtaka dhidi ya vyama vya Chadema na CUF, kutokana na madai ya kukiuka taratibu za uchaguzi wakati wa urudishaji fomu za wagombea wao katika uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Igunga.

 Mbali ya kufungua jalada hilo, jeshi hilo pia limetoa onyo kwa vyama hivyo kuhusu mabaunsa wao na kuwataka wahakikishe wanafanya ulinzi kwa kufuata utaratibu, sheria na kanuni zilizowekwa.
 Mkuu wa Operesheni Maalumu wa Polisi, Simon Sirro alisema walifungua jalada dhidi ya Chadema akidai kwamba baada ya kumaliza kurudisha fomu walifanya mkutano wa hadhara kinyume cha sheria.

 Juzi, mashabiki wa vyama vya Chadema na CUF walitunishiana misuli wakati wa urejeshaji fomu za wagombea wao kwenda Ofisi ya Tume ya Uchaguzi, hatua ambayo nusura isababishe ghasia na uvunjifu wa amani na baadaye Chadema kilifanya mkutano wa hadhara.

Stori zaidi soma Mwananchi

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...