September 20, 2011

CHADEMA YAPETA DHIDI Ya MADIWANI WALOTIMULIWA


MAHAKAMA ya hakimu mkazi Arusha imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na madiwani watano waliofukuzwa kwenye Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambapo imedaiwa kuwa madiwani hao wanatakiwa kulipa garama mbalimbali ambazo zimetumika katika kesi hiyo.

Hapo awali Madiwani hao waliwasilisha pingamizi ambapo pingamizi hilo lilidai kuwa madiwani hao hawakutendewa haki na chama hicho ambapo chama hicho kiliwafukuza .
hayo yamedhibitika leo,(JANA) katika mahakama ya hakimu mkazi ya jiji la arusha ambapo kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Hawa Mguruta ambapo alisema kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kupitia hoja nne za pingamizi zilizowasilishwa mahakamani hapo na mawakili wadaiwa , Method Kimomogoro na Albert Msando na majibu ya wakili wa wadai ,, Severine Lawena .

Katika shauri hilo la madai namba 17 la mwaka 2011 washitakiwa walikuwa ni Chama Cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA) na Freeman Mbowe huku wadai wakiwa ni madiwani waliofukuzwa kwenye chama hicho na kata zao kwenye mabano ni Naibu Meya , Estomii Mallah ( Kimandolu) , John Bayo (Elerai), Ruben Ngowi ( Themi), Rehema Mohamed (Viti Maalum) na Charles Mpanda (Kaloleni).

Aidha Hakimu Mguruta alisema kuwa anakubaliana na hoja za mawakili wa wadai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kuchunguza maamuzi ya chombo binafsi kama ilivyo kamati kuu ya Chadema ambapo walibainisha kuwa chombo chenye mamlaka hayo ni mahakama kuu .

"ni kwamba nakubaliana na hoja kuwa Chadema haiwezi kushitakiwa kwa jina lake kwani jina hilo halina uhai kisheria hivyo haiwezi kushitaki wala kushitakiwa kwa mujibu wa sheria'alieleza Hakimu Mguruta.

Hakimu Mguruta alisema kuwa anakubaliana na hoja ya mawakili hao kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho (Mbowe) hawezi kushitakiwa binafsi alipaswa kushitakiwa kwa nafasi yake ua Uenyekiti wa Taifa vinginevyo hataweza kutekeleza maelekezo ya mahakama hiyo ndani ya Chadema

“Mbowe alipaswa kushtakiwa kwa nafasi yake ya uenyekiti wa Taifa kwani endapo ataondolewa kwenye nafasi hiyo au kujiuzulu hataweza kutekeleza maamuzi ya mahakama kwani hataweza kuendesha na kusimamia maamuzi ya vikao ndani ya chadema” alisema hakimu mguruta .

Katika hatua nyingine Hakimu huyo alikubaliana na hoja kuwa kesi hiyo imefika mahakamani hapo ikiwa imepitwa na wakati kwani tayari madiwani hao walishakata rufaa kwenye baraza kuu la Chadema hivyo kesi hiyo imepoteza maana huku akiongeza kuwa mahakama kuu ndiyo yenye uwezo wa kupitia maamuzi yaliyofanywa na na vikao ndani ya taasisi lakini haiwezi kuhoji au kuamua juu ya taratibu za ndani za chama husika .

Wakati maamuzi hayo yakitolewa madiwani watatu kati ya watano waliofungua kesi hiyo walikuwa mahakamani hapo ambao ni Diwani wa kata ya Elerai Bw John Bayo , Naibu Meya wa jiji la Arusha ambaye pia ni diwani wa a kata ya Kimandolu, Bw Estomih Mallah ambapo walipotakiwa kutoa maoni yao mara baada ya kikao cha mahakama kumalizika walisema kuwa hawana maoni ya kuongea na vyombo vya habari. .

Aidha iliwabidi madiwani hao waliofungua kesi hiyo kusubiri ndani ya chumba cha mahakama mpaka mashabiki hao wa Chadema walipotoka nje ndipo nao wakatoka ingawa waliendelea kukaa kwenye maeneo hayo ya mahakama mpaka wanachama hao walipoondoka kwa maandamano na mbunge wa Arusha Mjini , Godbless lema .

Hata hivyo katika hatua nyingine polisi wenye silaha na mabomu ya machozi wakiwa kwenye magari mawili ya Polisi yenye namba za usajili PT 1844 na PT 0746 walifika na kuwaamuru wanachama hao kutawanyika mbele ya jengo la ofisi za mkuu wa wilaya ya Arusha zilipo ofisi za mbunge huyo ambapo walitii na kuondoka .

Story kwa hisani ya Full Shangwe Blog

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...