Dayosisi moja mjini Los Angeles, Marekani, imemchagua askofu, na ambaye waziwazi inafahamika anahusishwa na mapenzi ya jinsia moja.
Huyu ni askofu wa pili katika kanisa la Anglikana na anayehusishwa na mapenzi ya jinsia moja, jambo ambalo limesababisha mgawanyiko mkubwa katika kansia hilo.
Mchungaji Mary Glasspool, kutoka Baltimore, alichaguliwa kama askofu msaidizi, ingawa anahitaji kuungwa mkono na kanisa la Episcopal (Anglikana) nchini Marekani ili kikamilifu kukabidhiwa mamlaka hayo.
Gene Robinson (pichani) alikuwa wa kwanza kuchaguliwa kama askofu wa mapenzi ya jinsia moja, katika dayosisi ya New Hampshire, miaka sita iliyopita, na jambo hilo likasababisha mgawanyiko katika kanisa Anglikana.
source: BBC
1 comment:
jamani ndo kiama kimeshafika hivooooo!
Post a Comment