Akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, ambaye ni Mbunge wa Wawi (CUF), kwa uchungu, Pinda alisema kauli aliyoitumia ni katika kuwahakikishia wauaji hao kuwa Serikali sasa imechoshwa na unyama wanaoufanya na wasidhani Taifa na Watanzania watawavumilia.
“Pengine kuna mtu ambaye hajapata nafasi ya kuonana ana kwa ana na kuzungumza na watu hawa (albino), mimi nimekutana nao nimeona jinsi wanavyoumia (analia), mimi nilisema kuwa wauaji hawa hawawezi kuvumiliwa,” alisema Waziri Mkuu huyo na kukatisha kidogo hotuba yake na kulia.
Huku akifuta machozi, aliendelea kusema iwapo kuna Mtanzania ambaye anaona kuwa ametenda uovu kuliko maovu yote katika suala hilo la albino na iwe hivyo, lakini nia yake ilikuwa nzuri. Alisema alianza ziara yake katika Mkoa wa Tabora, baada ya kupewa kiundani historia ya mauaji hayo ambayo yalianzia kwa vikongwe ambao kwa takwimu alizopewa, waliouawa kwa mapanga walifikia 2,000 kwa sababu za kishirikina.
Alisema wakati mauaji hayo yakiendelea kukemewa, mwaka 2006 yalianza mauaji ya albino kwa kasi ndogo, lakini hadi juzi akiwa katika ziara hiyo, alipewa takwimu kuwa walifikia 28 na wengine watatu wakauawa akiwa bado katika ziara hiyo.
Aliongeza kuwa kwa watu ambao wameyashuhudia mauaji hayo, si mazuri na ni ya kutisha kwa kuwa wauaji wanachotaka ni viungo. “Tukio la Januari 22 wenyewe mliona yule baba wa watu alipokatwa mguu wa kulia na kisha kutelekezwa hapo, damu ilimwagika hadi akafa.” Alisema pamoja na Tanzania kusifika ndani na nje ya nchi kuwa ni nchi yenye amani na utulivu, mauaji hayo sasa yameitia doa nchi.
“Kutokana na mazingira haya, niliamua kufanya ziara na katika ziara yangu nilisisitiza umuhimu wa vyombo vya Dola katika kudhibiti mauaji haya, elimu kusambazwa kwa wananchi, kuongezwa kwa huduma za afya, madhehebu ya dini kukemea mauaji hayo na vyama vya siasa kuungana katika kupambana na tatizo hilo,” alisema.
January 30, 2009
Kilio cha Mtu mzima.......
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH

The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
WINNERS Boulevard.: Biashara ya Masoko ya Mtandao : Fikiria kama ungekuwa walipwa kwa kila ushauri wa kutumia huduma ama bidhaa ya kampuni a...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
Jessica is recognized internationally as an inspirational keynote speaker. Born without arms, Jessica now flies airplanes, drives c...
-
Mv Spice. Photo by AFP Waziri wa Mambo ya Ndani Nahodha akiangalia uokoaji. Waokoaji wakiwa na baadhi ya miili iliyoopolewa, mpaka...
-
But while the suspect was being attended to in one of the wards at Leratong Hospital in Krugersdorp, west of Johannesburg, the on-...
-
Gadhafi na Obama With reported pockets of fighting remaining in Tripoli on Wednesday, the whereabouts of Lib...
-
Miili ya Walter na Vonetha wakati wa ibada ya mazishi Leaders Club. Ilikuwa ni simanzi na majonzi wakati Baba mzazi wa Walter Capt George M...
-
Miaka mitano ni michache sana kwa mwanadamu, ni umri ambao mtoto kama atakuwa ameenda vyema basi atakuwa chekechea ambapo atatarajia kuk...
No comments:
Post a Comment