Kumekuwa na mjadala ama kutupiana lawama pengine kutafuta mchawi wa sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu cha wanafunzi hasa kidato cha nne, twawweza kutafuta mchawi kila mahali, kuanzia kwa wanafunzi wenyewe, walimu, serikali, wazazi na hata jamii kwa ujumla lakini bado haitasaidia hata kama tutapata kwamba mchawi wetu ni fulani.
Kwa hakika kila mmoja wetu ana sehemu katika hili japo kwa asilimia kubwa serikali yaweza kuwa ndo yachukua mzigo wa lawama, kuna mifano kadhaa.
Kwa mfano majuzi nimekutana na wanafunzi wanasoma Mbweni Sekondari karibu na bagamoyo lakini wanatoka Mwananyamala na Mbagala, ni shule za serikali hizi, hawa walinikumbusha wale niliokutana nao wanatoka Mbagala na wanasoma Mapinga.
Wanafunzi hawa kwa siku wanatumia mabasi yasiyopungua sita kwenda na kurudi, ina maana kuwa kwa siku wanakumbana na maudhi, manyanyaso na pengine matusi na kashfa za makonda wasiopungua sita,mbali na adha ya kuamka saa kumi usiku na kurudi nyumbani kuanzia saa mbili ama tatu usiku, kwa wiki ina maana wanakumbana na kadhia hii mara 36 je kwa mwezi, na mwaka je? mtoto huyu tunatarajia atakuwa na maendeleo gani kimasomo?
Ni kweli kuwa watoto wote wanapaswa kwenda shule lakini je hata kama kwa mazingira kama haya kweli? elimu hii tunayompa ambayo muda wake mwingi wapotelea kwenye madaladala ni elimu bora kweli au bora elimu?
Wizara ineangalia upya utaratibu huu wa wanafunzi kufaulu na kuwapeleka mbali kabisa na maeneo yao kwani ni usumbufu mkubwa kwa wanafunzi na maendeleo ya elimu na taifa kiujumla.
Naamini hii nayo ni moja kati ya sababu nyingi zinazochangia kuporomoka kwa kasi kwa elimu yetu hapa bongo.
No comments:
Post a Comment