October 4, 2011

Zanzibar UPDATES- Kampuni za Bima kulipa fidia.




KAMPUNI za bima nchini chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Bima Tanzania, zimekubaliana kulipa fidia kwa madai yoyote yatakayowasilishwa kuhusu vifo, waathirika na majeruhi wa ajali ya Mv Spice Islanders iliyotokea Desemba 10, mwaka huu.


Akiwasilisha mchango wa Sh10 milioni, kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bima Tanzania, Profesa Mgongo Fimbo, alisema kampuni hizo zimekubali kulipa madai yatakayotokana na ajali hiyo.



Profesa Fimbo alisema uamuzi huo ulifikiwa na kampuni hizo baada ya kuzingatia zaidi sababu za binaadamu, hivyo kitakachohitajika kwa wahusika ni kuwa na vielelezo kamili.


“Wale waliofiwa watalazimika kuwa na uthibitisho wa vifo unaotolewa na mamlaka inayohusika, wakati waathirika na walemavu watalazimika kuwa na vyeti vya daktari,” alisema Profesa Fimbo.


Alisema kwa mujibu wa Sheria za usafiri wa baharini, meli yoyote iliyosajiliwa Zanzibar lazima iwe na bima.

Profesa Fimbo alisema meli ya Mv Spice ingawa haikuwahi kulipa bima kipindi cha mwezi mmoja kabla ya kuzama kwake, bado bima ya meli hiyo inaonekana ina utata kidogo.



Alisema kampuni hizo zitahusika na ulipaji bima hiyo, huku taratibu za malipo hayo zikiangaliwa kwa kina.

Akipokea mchango huo, Balozi Iddi aliendelea kuzishukuru taasisi na jumuiya tofauti zinazochangia mfuko huo kwa lengo la kuwafariji wananchi waliokumbwa na maafa ya kuzama kwa meli hiyo.

Source: Mwananchi

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...