JUKWAA la Wahariri Co Limited limetangaza kumfungulia Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni George Mkuchika baada ya kugoma kuandika habari zake kwa takribani miezi minne sasa.
“Tayari gazeti liko mitaani, tunatangaza kumfungulia Mkuchuka. Lakini pia tunalaani kitendo cha kutumia sheria mbovu kuvifungia vyombo vya habari,” alisema mwenyekiti wa jukwaa hilo Sakina Datoo. Hata hivyo jukwaa hilo lilikishambulia kituo cha televisheni cha ITV kuwa kilifikia hatua ya kurusha habari za waziri huyo hasa baada ya Mkuchika mwenyewe kuzungumzia habari zinamlinda mmiliki wa kituo hicho Reginald Mengi.
February 19, 2009
Jukwaa lakubali yaishe..
Liyumba atoweka????????
Wadhamini wa mshitakiwa Amatus Liyumba, Benjamin Nguluguni (kushoto) na Otto Agaton, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo baada ya kukamatwa kwa kukosekana mshtakiwa Liyumba.DHAMANA aliyopewa Amatus Liyumba imeingia dosari baada ya mahakama kutoa amri ya kukamatwa pamoja na wadhamini wake, lakini juzi na jana alisakwa na maafisa wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) lakini hakuonekana.
Alitakiwa apandishwe mahakamani jana, lakini badala yake maafisa wa takukuru waliambulia kuwakamata wadhamini na wakakiri mahakamani hapo kuwa Liyumba haonekani. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi ilitoa hati ya kukamatwa kwa Liyumba ikiwa ni siku moja tu baada ya kupewa dhamana na mahakama hiyo katika mazingira ambayo hayakuwaridhisha upande wa mashitaka. Hakimu Hadija Msongo jana alikiri kuwa mahakama hiyo ilitoa hati ya kukamtwa kwa mshitakiwa huyo pamoja na wadhamini wake. Hata hivyo hakueleza sababu ya mahakama kutoa hati hiyo kwa kile alichodai kuwa jalada la kesi hiyo tayari limepelekwa mahakama kuu. Ifate hapa baadaye.
Dk Kitine: AZOZA.
MKURUGENZI Mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa, ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Makete na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), katika serikali ya awamu ya tatu, Dk Hassy Kitine ameonya kwamba, uchafu na wizi mkubwa wa rasilimali za taifa, mustakabali mbaya wa kisiasa na hali ngumu ya uchumi vinavyoikabili nchi, vinahatarisha usalama wa taifa.
Kauli ya Dk Kitine ambaye alishika wadhifa huo wa Ukurugenzi katikaIdara ya Usalama wa Taifa, wakati serikali ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, imetolewa wakati nchi ikiwa imegubikwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya ufisadi na vita ya chini kwa chini ya kugombea madaraka.
Akizungumza katika mkutano maalumu na baadhi ya vyombo vya habari katika mgahawa wa Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam jana, Dk Kitine alionya kwamba, uchumi na maliasili za taifa zimeshikwa na wageni, huku Watanzania walio wengi wakifanya kazi za udereva, ufagiaji barabarani, kazi za ndani na mashambani. "Nimewaiteni kuzungumzia mustakabali wa nchi yetu, kama mnavyofahamu mimi nimeshika nafasi mbalimbali nyeti kuanzia wakati wa Mwalimu," alifahamisha. ICHEKI HAPA.
KP NA WENYE NACHO
Liyumba atoweka??????
TUNGALI TUNAFUATILIA MAHAKAMANI KISUTU TUTAWAJULISHA TAARIFA KAMILI ZAIDI SI MUDA.
DEMOKRASIA
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Nimekuta ubishi paala fulani tena kwa watu naweza sema ni waelewa kiasi fulani maana wameenda shule na wengine wako katika fani, ati ile ho...
-
Prof Aloysius Mwessa Hnonoli ni Mbongo wa kwanza kuwa Mkurugenzi wa Muhimbili na Mkuu wa Chuo kikuu cha Tiba. Mstaafu huyu jana alitu...
-
WADAU NADHANI SI VIBAYA SIKU MOJA MOJA TUKAPANUA MAWAZO KIDOGO NDO NAMNA YA KUELIMISHANA KUPITIA NJIA HII. HIKI ni kijiji kipo hapa bo...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
Mgonjwa wa saratani akipata huduma Ocean Road Cancer Insititute (ORCI) asubuhi leo hii baada ya kununuliwa kwa vifaa vilivyokuwa vimeibwa y...
-
Mineral occurrence in Tanzania by TMAA UONGEZAJI WA PATO LA MTANZANIA Mheshimiwa Spika, 46. Lengo la Dir...
-
Shibe inapoua kuliko njaa Obesity kills more people than hunger Most of the world's populations live in countries where overweight a...
-
Dr H Mwakyembe akishushwa toka ktk ndege ya kukodi na kupelekwa moja kwa moja MOI kwa Matibabu zaidi, Dr Mwakyembe alipata ajali ya gari m...
-
Ukumbi huko nyuma ya Minara miwili ukiwa ni wa mviringo. Eneoe kubwa la chai na ukaguzi pamoja na usajili kwa waalikwa. Sehemu za waa...