March 31, 2009

Meli yakwama Dar

Meli kubwa ya makasha MSC Federica imekwama karibu na ufukwe wa Kigamboni ilipokuwa ikitoka bandari salama leo yapata saa kumi na dk 45 kwa kile inachodhaniwa kuwa ni kupoteza mwelekeo, juhudi za kuikwamua zinaendelea.

Bongo kupeleka kikosi Darfur mwezi ujao..

Msuluhishi wa Darfur Dkt Salim Ahmed Salim akiagana na mkuu wa kikosi cha JWTZ kitakachoelekea Darfur mwezi ujao Luteni Kanali Ally Katimbe leo katika kambi ya Jeshi hilo iliyoko Msata ,Pwani baada ya kutoa mhadhara kwa kikosi hicho kuhusu hali ya jimbo la Darfur.
MSULUHISHI wa Umoja wa Afrika (AU) katika mgogoro wa Darfur , Sudan, Dk. Salim Ahmed Salim leo amezuru kambi ya kikosi maalum cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania wapatao 875, kinachojiandaa kwenda kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan,
Askari hao na maofisa waowanatarajiwa kuondoka nchini mwezi huu kuelekea Sudan kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa.

Kuna watu wanaandika lakini huyu mhhh si mchezo..

How dare you Idris Rashid???
"THE mistake a lot of politicians make is forgetting they’ve been appointed and thinking they’ve been anointed," remarked US Senator Claude Pepper (1900-1989) Democrat.
Pepper reached this conclusion after finding that many people with appointive positions erroneously turned them into personal estate.
I heard Dr. Idris Rashidi, TANESCO Managing Director, saying: "If we refuse to buy hand-me-down Dowans' generators, our country would sink ................more here

WANAMEREMATAAA WANA.......................

Hongera sana kwa kutimiza miaka 2o ya ndoa Mh Rais JK na Mama Salma.

March 30, 2009

Saba wathibitika kufa ajali ya treni Dom.

MAITI za watu waliokufa katika ajali ya treni iliyotokea katika kitongoji cha Pandambili, katikakati ya stesheni ya Gulwe na Igandu hazijatambuliwa hadi kufikia hii leo.
Kulingana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma , William Lukuvi jumla ya watu saba ndio waliofariki katika ajali hiyo na wengine saba kujeruhiwa.
Lukuvi alisema kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali kuu ya mkoa wa Dodoma ambapo maiti hizo zimeshindwa kutambuliwa kutokana na majina yaliyoandikwa katika tiketi zao kutokamilika..

RIP Hamidu Bisanga

Mazishi ya Marehemu Hamidu Bisanga (59) mwandishi wa habari wa siku nyingi aliyefariki dunia jana kwa ajali ya gari katika eneo la Kijitonyama karibu na Millenium Tower yanatarajiwa kufanyika kesho ktk makaburi ya Kisutu. Katika Uhai wake, Bisanga alifanya kazi kama Mhakiki wa lugha katika kiwanda cha Printpak mwaka 1973 hadi 1975 na baadaye katika Magazeti la Serikali ya SundayNews na DailyNews kuanzia mwaka 1975 hadi 1990 akiwa mwandishi wa habari na baadaye mwaka 1990 hadi 1994 alifanya kazi katika magazeti hayo akiwa Msanifu Mkuu.

Mwaka 1994 hadi 1998 aliajiliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kama Afisa uhusiano na mwaka 1998 aliajiliwa na Shirika la Maendeleo (NDC) akiwa Meneja uhusiano hadi August mwaka jana alipohamia katika Kampuni ya BayPort kuwa Meneja Uhusiano na Masoko.

Pia Marehemu Bisanga aliishawahi gazeti la African, Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC),Sauti ya America na wakala wa Habari wa Ufaransa.

March 28, 2009

Kilwa Road "mukide"

Barabara ya Kilwa yaelekea kukamilika hivyo kupunguza (au kuongeza) usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii hasa wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake.
Pamoja na juhudi na nia njema za serikali kutengeneza miuondo mbinu ya jiji letu hili ambazo hazina budi kupongezwa lakini nna pata mashaka na maafisa mipango wetu (Kama kweli tunao) jinsi au namna ya vile miradi hii ambavyo anapangwa au kutekelezwa.
Hebu tuangalie barabara hii na ile ya Mandela jinsi vile zajengwa leo hii, mi nadhani dizaini hii ni ya miaka ya 70 na si elfu mbili na ushee kwani sidhani kuwa kwa msongamano huu unaokua kila uchao bado twaitaji barabara za njia nne zisizozingatia watumiaji wengine mbali na wa vyombo vya moto.
Barabara zote hizi hazina njia ya waendesha baiskeli yaani haipashwi kuchanganya baiskeli na waenda kwa miguu bali kila mmoja awe na njia yake, nadhani yawezekana Bongo ndo sehemu hatari zaidi kwa watumiao ingini kiuno kuliko sehemu zinginezo, na kwakweli usafiri huu bado wafaa na watumika sana nchi za wenzetu zilizoendelea mpaka leo hii kama picha hizi hapa zioneshavyo.

March 27, 2009

JK achekecha Ma DC

  • Saba wastaafishwa,

  • 15 waingia,

  • 54 wahamishwa,

  • 2 kiporo

  • Ngulume, Mashimba, Maarugu, Dololo, Holela, Madaha nje

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya kwa kuteua wapya 15, kustaafisha saba na kuwabadilisha vituo 54.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), ilionyesha pia kuwa wakuu wa wilaya wawili watapangiwa kazi nyingine na wengine wawili wameondolewa baada ya hivi karibuni kuteuliwa kuongoza Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wakuu wapya na wilaya zao kwenye mabano ni Mercy Silla (Arumeru), Norman Sigalla (Hai), Kanali Issa Njiku (Misenyi), Angelina Mabula (Karagwe), Dk. Rehema Nchimbi (Newala), Francis Isaac (Mbulu), Luteni Kanali Benedict Kitenga (Rorya) na Luteni Kanali Cosmas Kayombo (Mbarali).

Wengine ni Christopher Kangoye (Kwimba), Queen Mlozi (Ukerewe), Fatuma Mwassa (Mvomero), Fatma Ally (Nanyumbu), Juma Madaha (Tunduru), Anatory Choya (Kishapu) na Erasto Sima (Korogwe).

Zaidi tembelea hapa

Mwaka wa hasara.............

Gari alilokuwa akiendesha Mzee wa "Vijisenti"
Hii ndo Bajaj. Mzee wa "Vijisenti" Andrew Chenge (kulia) akiwasimulia Maofisa wa Polisi, Naibu DCI Peter Kivuyo (katikati) na Kamanda wa Trafiki Kanda maalum ya Dar es Salaam Mohamed Mpinga namna ambavyo ajali ilitokea baada ya gari alilokuwa akiliendesha kugongana na bajaji na kusababisha vifo vya wanawake wawili ambao wanadaiwa kuwa walikuwa wakitoka kujirusha klabu Maisha usiku wa kuamkia leo Oysterbay Dar es Salaam.

"Mwaka wa hasara ni hasara"

Wahenga walisemaga zamani kuwa mwaka wa hasara basi uwa ni hasara tu, hata ukipanda mchicha kwa nia nzuri kabisa ya kusevu bajeti ya mboga basi uota bange.
Mhh pole sana Mh "Vijisenti"

March 25, 2009

"Wajinga ndo waliwao" Lini tutaelimika???

Report: African countries losing millions
Poor African countries rich in minerals are losing tens of millions of dollars in revenue that can be used to fund health, education and other social programs because of tax breaks and low royalties they have given to mining companies, said a report released Wednesday.
The mining companies have been given tax concessions or low royalty rates because the contracts signed with the governments have been negotiated in secret or government ministries have wide discretionary powers that lawmakers have no say over, said the report.
Titled "Breaking The Curse," the report is the work of a coalition of international and local non-governmental organizations that includes Actionaid International and Christian Aid. It covers seven Africa countries: Congo, Ghana, Malawi, Sierra Leone, South Africa, Tanzania and Zambia.
The report estimates low royalty rates have or will cost South Africa, the continent's biggest gold producer, up to $359 million a year in revenue. Similarly, another top African gold producer, Ghana, is losing $68 million a year in revenue, and Tanzania, the continent's third largest producer, $30 million a year in income, the report said.
"African mining tax regimes need to be reformed to ensure that African governments are able to collect a fair share of mining rents to fund their national development plans," said the report.
"In some countries this would require an increase in the rates of royalties and other taxes; in others this would require a stop to the practice of negotiating tax breaks for individual companies in secret contracts."

The report points out that the seven African countries covered have lost the chance to collect huge sums of revenue at a time when global prices for metals are coming out of a five-year boom that ended last year.
HIVI SISI WAAFRIKA TUMEROGWA NA NANI? KILA SIKU KIGUU NA NJIA KUOMBA KWA HAOHAO??
NA HAO VIONGOZI WETU AMBAO TULIWAAMINI NA KUWAKABIDHI MAJUKUMU ILI WATUWAKILISHE KATIKA MIKATABA FEKI HII TUWAFANYEJE?? INASIKITISHA SANA HII.

March 24, 2009

Ufuska wa walimu ka ni kweli bye bye....

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro , Said Mwambungu ( mwenye suti) akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Lupanga mara baada ya kumaliza mazungumzo na walimu wa shule hiyo kuhusiana na mgomo wa wanafunzi na kuwataka warejee madarasani wakati uchunguzi wa kina dhidi ya walimu walioongoza kupigiwa kura za maoni ukiendelea kwa ajili ya kuchukua hatua za kinidhamau naa kisheria.
Ikibainika ni kweli waliohusika uenda wakafukuzwa kazi- CWT
Na Theopista Nsanzugwanko
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimesema iwapo itathibitika kuwa walimu watano wa kiume katika Sekondari ya Lupango wamekithiri katika vitendo vya ngono na wanafunzi wa kike wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kufukuzwa kazi.

Aidha,ametaka uchunguzi wa kina ufanyike isiije ikawa ni chuki binafsi za watu wenye nia ya kutaka kuwaaribia sifa walimu.

Akizungumza na Habari Leo, Rais wa Chama cha Walimu Nchini (CWT), Gratian Mkoba alilaani kitendo hicho ambacho kinaendana kinyume na maadili ya ualimu na kusisitiza kuwa yeye hana uhakika na jambo hilo lakini kama ikigundulika wachukuliwe hatua.

“Sisi hatufurahishwi na kitendo hicho kilichoizalilisha kazi ya ualimu,kwani tunaamini kuwa kuwa walimu ambao hawana taaluma ya ualimu bali wameingia tu katika fani hii hivyo wachukuliwe hatua kali ikibainika hata kufukuzwa kazi”alisema Mkoba

MSAFIRI KAFIRI

Usafiri wa wanafunzi ktk jiji hili umekuwa ni kasheshe kiasi cha watu wenye malori, japo yamepakia mzigo kulazimika kuwaonea huruma na kuwasaidia, lakini nadhani tutakubaliana kuwa hii si njia njema ya usafiri na pia ni hatarishi na je iwapo litatokea la kutokea (Mungu apishie mbali) tutamlaumu nani? tutamnyooshea nani kidole? Hivi yale mabasi au mradi wa wanafunzi ulikufakufaje vile? maana hata screpa zake sizani kama zaweza kuonekana! Je nini kifanyike kabla mambo hayajaharibika??

JK aenda visiwa vya Comoro

Rais Jakaya Kikwete akiagana na Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mizengo Pinda au"Mtoto wa Mkulima" na viongozi mbalimbalia katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda Comoro ambako atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu.

March 23, 2009

Mpiganaji Athumani yuko fiti

Mpiganaji Athumani Khamisi akijuliwa khali na Ikunda Erick na Mama "Bhoke" au Mkami huko bondeni alikolazwa,

Paradise, Oceanic finito"

Hotel za kitalii za Paradise na Oceanic zimeteketea kwa moto leo hii.

Moto Moto Motooooooo

Zim sasa mkate wanunulika

Toka kuanza kwa serikali ya umoja khali mjini Harare yarejea taratibu na vitu angalau sasa vinapatikana maduka na mkate nao si haba waweza nunulika japo ni kwa dola ya US.

March 22, 2009

Kilele cha wiki ya Maji leo

Leo ni kilele cha wiki ya maji ambapo kitaifa inafanyika Bukoba, Hapa ni Vingunguti Kwa Kombo ambapo wakazi wa hapa hujipatia maji kwa matumizi mbalimbali.

March 21, 2009

Zana Haramu za uvuvi zateketezwa BK

Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein akichoma moto zana haramu za uvuvi zilizokuwa zikitumiwa na baadhi ya wavuvi wanaovuwa kwenye ziwa Victoria zilizokamatwa kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Kasenda Wilaya ya Chato. Jumla ya Mitumbwi 23 na Nyavu 649 zilikamatwa na kuteketezwa hii leo.

UMASKINI WA JUMA NATURE ULIVYOGAWANWA

Kaaaaazi kweli kweli.....

March 20, 2009

Lipumba aunga mkono ununuzi wa Dowans

Prof Lipumba aungana na hoja ya Zitto.
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ametetea uamuzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutaka kununua mitambo iliyotumika ya kufua umeme.
Lipumba amesema uamuzi wa kununua ‘mitumba’ si mbaya ila cha kuzingatiwa ni kama mitambo itakayonunuliwa itakuwa na manufaa kwa nchi.
Hoja hiyo ni sawa na iliyotolewa na kusimamiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye alisema ununuzi wa mitambo ya Kampuni ya Dowans Limited, unazingatia maslahi ya Taifa, licha ya sheria ya manunuzi kuzuia.

Hizi ndo zile bike zilizojaa mitaani mwetu au???

Unclaimed bikes off to Tanzania
An African charity run by a Faughart priest got a boost last week thanks to Dundalk Gardaí – and a bunch of unclaimed bikes.
Bikes, which have been sitting at the station for months, have been given to Fr Christy McElwee for his Tanzanian communitybuilding charity.
Gardaí made a police property application to Dundalk District Court last week asking that the bikes be given to Fr McElwee for his charity.
The bikes will make a huge difference to the people of rural Tanzania, according to Fr McElwee, who got involved in the Rosminian Order-led charity about five years ago.
But it will take some more fundraising to get the much-needed bicycles to their final destination.

Nani anasababisha migogoro ya ardhi??

Wakazi wa Kwembe Kati wakizuia kwa shuka afisa wa upimaji ardhi kupima tena maeneo yao.
Pamoja na kuwepo askari wapatao ishirini wengine wakiwa na mitutu bado wananchi walikuwa ngangari kuakikisha kuwa hakuna upimaji wowote utakaofanyika tena pasipo kupewa somo kwanini wanapimiwa tena maeneo yao.
WAKAZI wa Kwembe Kati, Dar es Salaam wameendelea kuwazuia Maofisa Ardhi kupima viwanja katika eneo lao baada ya polisi zaidi ya 20 kutawanywa katika eneo lao ili wasimamie upimaji huo badala ya kutumia kamati ya wananchi kama walivyokubaliana.
Awali wakazi hao waliwazuia watendaji hao kupima viwanja hivyo vilivyo katika mradi wa viwanja 600 juzi kwa kile walichodai kutumia polisi kulazimisha upimaji badala ya kuishirikisha kamati ya wakazi kama ilivyokubaliwa katika kikao cha pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya, Fabian Massawe, kamati na maofisa ardhi hao hivi karibuni.
Pia wakazi hao takriban 300 waliyo katika mradi huo kupitia kamati yao ya watu 10 walikubaliana na uongozi wa wilaya kupitia upya mapendekezo ambayo yanahusu fidia kwa wale ambao miundombinu kama barabara, zinapita katika maeneo yao na wenye hati tayari baada ya kuonekana wanapata viwanja vidogo kuliko makubaliano.
“Tulipeleka mapendekezo kumi ambayo yalipaswa kutolewa majibu kabla maofisa hawa hawajaja kuendelea kupima, tulitaka ufafanuzi kuhusu ramani inayotumika na namna ambavyo mipaka ya mawe inawekwa juu ya mipaka mingine, tulitaka hayo yarekebishwe lakini tunashangaa wanakuja na polisi,” alisema Jackton Manyerere mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.
“Tunampataka Kanuti (jina la kwanza ni Dioscory Kanuti-Ofisa Mipango Ardhi) atufafanulie ramani ipi inatumika maana tangu mwanzo tupo nae katika vikao na Mkuu wa Wilaya, kwa nini anatuchanganya hivi,” alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hilda Mushi ambaye ramani ya awali ilionyesha barabara inapita katikati ya nyumba yake.
Hata hivyo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Upimaji Milki Mijini, Saimon Katambi baada ya kuangalia ramani iliyokuwa inatumika, aligundua kuwa haikuwa ramani inayopaswa kutumika na ndipo alipotoa ramani halali ambapo Ndaki alipoagiza upimaji uendelee kwa ramani sahihi.
Sakata hilo lililodumu zaidi ya saa tisa, liliishia kwa wakazi hao kuwataka maofisa ardhi kukaa pamoja na kamati, Mkuu wa Wilaya na Waziri mwenye dhamana, John Chiligati, kupitia mapendekezo ya wananchi ili upiamji uendelee.
Kwembe Kati ni eneo muhimu sana kwa siku za usoni, je kwanini???
Kama jina lilivyo Kwembe Kati, ipo katikati ya miradi miwili mikubwa sana ya siku za usoni, upande mmoja ukiwa ni eneo la wa mji mpya wa Dar au "Setilite City" ambao utajengwa hapo Kibamba na mwingine ni Chuo kikuu cha Tiba cha muhimbili ambacho nacha kipo upande wa pili wa eneo hili ivyo kwa siku za usoni hii ni kama Magomeni au Kinondoni flani ivi.

March 19, 2009

JK arejea toka UK

Rais JK amerejea leo mchana toka ktk kikao cha maandalizi ya Mkutano wa G 20 unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa Nne huko UK.

March 17, 2009

WAMA YAPIGWA JEKI.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete Amepokea Hundi ya shilingi Milioni Tano 5M Kutoka waKiongozi wa African Diplomatic Spouses Group (ADSG) Bi Hawaida Kalo Mke wa Balozi wa Sudan. Katikati ni Mke wa Balozi wa DRC Bi Celina Juma. Msaada huo umetolewa Ili kusaidia shughuli za WAMA.

Watani mmemsikia First Lady???

Mama Salma Kikwete awataka wanaume wa mkoa wa Mara kuacha tabia ya kuwapiga wake zao
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wanaume wa mkoa wa Mara kuacha tabia ya kuwapiga wake zao bali wawasaidie kufanya mambo ya maendeleo ambayo yatawasaidia kujikwamua kimaisha.

Mama Kikwete aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya siku mbili ya uwekezaji na ujasiriamali iliyofanyika katika ukumbi wa uwekezaji uliopo mjini Musoma.

“Nilikuwa nasikia kuwa eti wanawake wa mkoa huu wakipigwa na wanaume zao ndiyo wanaonekana kuwa wanapendwa sana sasa sijui kama ni kweli au la, lakini kwa kuwa leo niko na nyinyi wenyeji wa Mara nitajua kama ni kweli ”, alisema.
Tatizo langu mi kwa watani zangu hawa ni hapo, je kinamama si wataona waume zao hawawapendi? nasikia eti ikipita wiki bila kupigwa mama wa kikulya uanzisha zogo mwenyewe na asipopata kichapo basi atarusha jiwe juu ya bati afu atakinga mgongo iliaangukiwe nalo ndo amani inarejea ndani ya nyumba, kweli hayo watani???

JK in UK 4 G20 MEETING

Rais Jakaya Kikwete akiwa na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa UK Bw Gordon Brown.

Miaka thenashara bila malipo kipawa

Wakazi wa Kipawa walikusanyika kwa siku 2 mbele ya ofisi za Mamlaka ya viwanja vya ndege kudai malipo ya nyumba zao ambazo zilitathminiwa yapata miaka kumi na mbili iliyopita na kutakiwa wasizitengeze wala kufanya chochote hadi watakapolipwa mafao yao, uvumilivu umewashinda ilibidi wahamie ofisi za TAA ili kupeleka kilio chao.
Hatimye mkuu wa wilaya alihaidi kuwasaidia kufikisha kilio chao mbele kwa mbele kwani alikili kuwa hilo ni zito kwake kulishughulikia.

March 16, 2009

WAWEZA JUAJE KUWA PC YAKO IMEINGILIWA NA VIRUSI??

How to tell, what to do if computer is infected
Computer-virus infections don't cause your machine to crash anymore. Nowadays, the criminals behind the infections usually want your computer operating in top form so you don't know something's wrong.
That way, they can log your keystrokes and steal any passwords or credit-card numbers you enter at Web sites, or they can link your infected computer with others to send out spam.
Here are some signs your computer is infected, tapped to serve as part of "botnet" armies run by criminals:
• You experience new, prolonged slowdowns. This can be a sign that a malicious program is running in the background.
• You continually get pop-up ads that you can't make go away. This is a sure sign you have "adware," and possibly more, on your machine.
• You're being directed to sites you didn't intend to visit, or your search results are coming back funky. This is another sign that hackers have gotten to your machine.
So what do you do? • Having anti-virus software here is hugely helpful. For one, it can identify known malicious programs and disable them. If the virus that has infected your machine isn't detected, many anti-virus vendors offer a service in which they can remotely take over your computer and delete the malware for a fee.
• Some anti-virus vendors also offer free, online virus-scanning services.
• You may have to reinstall your operating system if your computer is still experiencing problems. It's a good idea even if you believe you've cleaned up the mess because malware can still be hidden on your machine. You will need to back up your files before you do this.
How do I know what information has been taken?

• It's very hard to tell what's been taken. Not every infection steals your data. Some just serve unwanted ads. Others poison your search result or steer you to Web sites you don't want to see. Others log your every keystroke. The anti-virus vendors have extensive databases about what the known infections do and don't do. Comparing the results from your virus scans to those entries will give you a good idea about what criminals may have snatched up

WAWEZA KISIA NINI KILITOKEA USIKU WA JANA YAKE?

Ukiangalia hii clip je waweza kisia nini hasa kilijili au tokea usiku wa jana yake hata mzee mzima "kulazimishwa" kusema au kuukana ukweli au uwongo?

March 14, 2009

RIP Faustine Kabuzi Rwilomba

Maafisa wa jeshi wakitoa nje ya kanisa jeneza lenye mwili wa Marehemu Rwilomba kuelekea eapoti tayari kwa mazishi huko kijijini kwake ktk wilaya ya Geita mkoa wa Mwanza kesho. Wasifu wake ni huu.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...