March 17, 2009
WAMA YAPIGWA JEKI.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete Amepokea Hundi ya shilingi Milioni Tano 5M Kutoka waKiongozi wa African Diplomatic Spouses Group (ADSG) Bi Hawaida Kalo Mke wa Balozi wa Sudan. Katikati ni Mke wa Balozi wa DRC Bi Celina Juma. Msaada huo umetolewa Ili kusaidia shughuli za WAMA.
Watani mmemsikia First Lady???
Mama Salma Kikwete awataka wanaume wa mkoa wa Mara kuacha tabia ya kuwapiga wake zao
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wanaume wa mkoa wa Mara kuacha tabia ya kuwapiga wake zao bali wawasaidie kufanya mambo ya maendeleo ambayo yatawasaidia kujikwamua kimaisha.
Mama Kikwete aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya siku mbili ya uwekezaji na ujasiriamali iliyofanyika katika ukumbi wa uwekezaji uliopo mjini Musoma.
“Nilikuwa nasikia kuwa eti wanawake wa mkoa huu wakipigwa na wanaume zao ndiyo wanaonekana kuwa wanapendwa sana sasa sijui kama ni kweli au la, lakini kwa kuwa leo niko na nyinyi wenyeji wa Mara nitajua kama ni kweli ”, alisema.
Tatizo langu mi kwa watani zangu hawa ni hapo, je kinamama si wataona waume zao hawawapendi? nasikia eti ikipita wiki bila kupigwa mama wa kikulya uanzisha zogo mwenyewe na asipopata kichapo basi atarusha jiwe juu ya bati afu atakinga mgongo iliaangukiwe nalo ndo amani inarejea ndani ya nyumba, kweli hayo watani???
Miaka thenashara bila malipo kipawa
Wakazi wa Kipawa walikusanyika kwa siku 2 mbele ya ofisi za Mamlaka ya viwanja vya ndege kudai malipo ya nyumba zao ambazo zilitathminiwa yapata miaka kumi na mbili iliyopita na kutakiwa wasizitengeze wala kufanya chochote hadi watakapolipwa mafao yao, uvumilivu umewashinda ilibidi wahamie ofisi za TAA ili kupeleka kilio chao.
Hatimye mkuu wa wilaya alihaidi kuwasaidia kufikisha kilio chao mbele kwa mbele kwani alikili kuwa hilo ni zito kwake kulishughulikia.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
Shibe inapoua kuliko njaa Obesity kills more people than hunger Most of the world's populations live in countries where overweight a...
-
LONDON (Dow Jones)--U.K. defense giant BAE Systems PLC (BA.LN) Tuesday was fined GBP500,000 for improper accounting in relation to the award...
-
On Tuesday, 7th July we witnessed the peak of the Saba Saba festivities. I never go to the Dar es Salaam International Trade Fair, these day...
-
HII NI HOSTEL YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI WANAPOISHI WATAALAMU WETU WA AFYA WA KESHO.
-
The Himba are an ethnic group of about 20,000 to 50,000 people living in northern Namibia, in the Kunene region (formerly K...
-
WADAU NADHANI SI VIBAYA SIKU MOJA MOJA TUKAPANUA MAWAZO KIDOGO NDO NAMNA YA KUELIMISHANA KUPITIA NJIA HII. HIKI ni kijiji kipo hapa bo...