May 31, 2010

"Kilimo Kwanza" Zana zinapokwishne

Zana za kazi "kilimo kwanza" hapnshaka watumishi hii pale Lindi mjini ni waumini wazuri wa PSI isipokuwa bosi tu ndo anajisahau kujaza upya stoku.

May 28, 2010

DARASA LILIPOKOLEA

Nikitoa darasa la picha na mtandao kwa washiriki wa mkoa wa Lindi hivi karibuni, sometimes si vibaya ku-share kile ukijuacho na wengine kwa faida ya Bongo yetu njema tutakayo kuijenga.

May 24, 2010

Masikini Liyumba! alamba mvua mbili

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu leo hii imemuhukumu aliyekuwa DAP wa BOT Amatus Liyumba kwenda miaka 2 jela kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka akiwa mtumishi wa umma.

Lindi at Sunrise

Hii ni taswira unakutana nayo majira ya saa moja na ushee hivi asubui nje tu ya hoteli tulo kuwa tumefikia kule Lindi Ufukoni Beach.

May 23, 2010

TWIGA STARS WAWACHAPA ERITREA 8 - 1

TIMU ya soka ya wanawake Twiga Stars jioni hii imewachapa bila huruma timu ya Eritrea katika mechi ya kwanza ya ngwe ya mwisho ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika zitakazopigwa Agosti mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Nangurukulu Public Toilet

May 20, 2010

Zaidi ya 20% waliofaulu hawajalipoti mashuleni mkoani Lindi

Wanafunzi 1897 kati ya 8491 waliochaguliwa kujiunga na shule za sekondari mkoani Lindi hawajalipoti mashuleni kwa mujibu wa taarifa ya mkoa.

May 19, 2010

Vigogo UVCCM Waachia ngazi

Mwenyekiti wa UV-CCM taifa Hamad Yusuph Masauni na Naibu katibu mkuu UV-CCM MOhamed Moyo wamejiuzulu nafasi zao wakidai kuwa wamefanya hivyo kwa maslahi ya umoja huo na chama cha mapinduzi. Viongozi hao wameandika barua hiyo ya kuitoa mbele ya kikao cha baraza kuu la vijana kilichomalizika majira ya saa nane usiku leo ,kikao kilichofunguliwa na katibu mkuu wa CCM Yusuph Makamba . kabla ya kujiuzulu Masauni alikuwa akituhumiwa kufoji cheti cha kuzaliwa huku Moyo akidaiwa kuendesha makundi ndani ya umoja huo .
kwa hisani ya Francis Godwin blog.

May 18, 2010

Lindi umeme in kasheshe

R - L Said Hamdan, Danstan Raphael, Mary Mpandula, Mwanzo Millinga na Kijakazi Yunus wakipitia baadhi ya assignments.

Greetings from Lindi

Hii ni kazi ya mmoja wa Waandishi wa habari toka mkoa wa Lindi waliokuwa ktk mafunzo ya upigaji picha yaliyokuwa yakitolewa na Flame Tree Media Trust.
Tembelea FTMT blog kwa picha zaidi.

May 14, 2010

Uvuvi haramu vs Mazingira

Ni kweli uvuvi haramu si mzuri na wa kupigwa vita popote Tanzania, lakini mazingira ya fukwe zetu nao si ni muhimu pia? uteketezaji wa nyavu hizi si wahitaji sehemu maalumu ili kuondokana na uharibifu wa mazingira katika fukwe zetu kama hii ya Ufukoni hapa Lindi?

May 12, 2010

Uvuvi Haramu

Waziri John Magufuri atet=keteza Nyavu haramu za kuvulia samaki huko Lindi.

David Cameron amrithi Brown

Kiongozi wa chama cha Conservative, David Cameron, ndiye Waziri Mkuu wa Uingereza baada ya Gordon Brown kujiuzulu Jumanne jioni.

May 11, 2010

Vick Ntetema ashinda tuzo ya kimataifa

Tanzanian journalist Vicky Ntetema has won an international award for her BBC reports on the murder of albinos.

The International Women's Media Foundation gave her a Courage in Journalism Award for her investigation.

"I am surprised but not happy," Ms Ntetema told the BBC, saying that a four-year-old boy with albinism had recently been killed.

Some Tanzanian witch doctors say magic potions made with albino body parts can bring good luck and wealth.

Some 53 people with albinism have been murdered in Tanzania in recent years, along with several others in neighbouring Burundi.

source: BBC

May 9, 2010

Hureeeeeeeeeeeee!!!!11

Wanasemaga "the winner takes it all", nilikuwa nikiwaambia mashetani wekundu lakini wabishi, waache na ubishi wao.

Kitimutimu cha Somanga, mhh we acha tu

Sio kama ndo naamka wadau, hapan hii ni baada ya kukata kipande korofi cha kiasi cha KM 60 maaarufu kama Somanga ktk barabara ya kuelekea kusini, twaambiwa tuna bahati maana hatukulala njiani, yasemekana watu wamalizaga wiki kukata kipande hiki, Mwanzo wa shughuri ni pale unapomaliza daraja la Mkapa.

May 8, 2010

Mpiganaji Athumani Hamis arejea

Umati wa wadau, ndugu jamaa, marafiki na zaidi wapiga picha wamelijitokeza leo hii kumlaki Kamanda Mpiganaji Athumani Hamis aliyerejea leo hii toka Afrika Kusini alikokuwa ameenda kwa matibabu.

Gazeti la Newsweek linauzwa!

For generations, Time and Newsweek fought to define the national news agenda every Monday on the newsstand. Before the Internet, before cable news, before People magazine, what the newsweeklies put on their covers mattered.

As the American conversation has become harder to sum up in a single cover, that era seems to be ending. The Washington Post Company announced Wednesday that it would sell Newsweek, raising questions about the future of the newsweekly, first published 77 years ago.

read more here

May 7, 2010

Mpiganaji Athumani kurejea Kesho

Mpiganaji Athumani Khamis anatarajiwa kurejea Bongo kesho saa 12 jioni na SAA toka Sauzi Afrika alikokuwa ameenda kimatibabu.
BP na wadau wote wanakuombea safari njema na karibu sana nyumbani.

May 5, 2010

Kikongwe apinga hotuba ya JK.

WAZEE zaidi ya 1,000 waliokuwa wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete juzi kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee walikuwa wakimshangilia mara kwa mara, lakini si Bi Asha Omary, 70, aliyekuwa kijijini kwake wilayani Kisarawe.

Kikongwe huyo alisikiliza hotuba hiyo, iliyobatilisha mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kuanza leo, kwenye redio akiwa Kijiji cha Bwana, Kata ya Kibuta na hasira alizopata kutokana na kauli za rais, zilimfanya aamue kusafiri takriban kilomita 35 kuanzia saa 1:00 asubuhi kuja jijini Dar es salaam kueleza jinsi alivyokerwa.

“Kama kiongozi wa taifa, rais angetumia maneno ya busara na hekima yasiyo na ukali ndani yake katika kutatua tatizo kwa sababu wafanyakazi wanadai haki yao na wanayo haki ya kufanya hivyo,” alisema Asha alipofika ofisi za gazeti la Mwananchi majira ya saa 4:30 jana.

“Rais amejisahau na anatumia vibaya mamlaka aliyopewa na Watanzania kuwakandamiza wafanyakazi, amesahau kuwa nafasi hiyo imetokana na wananchi wote wakiwapo hao wafanyakazi.”

Bi Asha alikuwa akizungumzia hotuba ya Rais Kikwete kuhusu mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kuanza leo, hotuba ambayo iliwashambulia viongozi wa Tucta kuwa ni "waongo, wanafiki, wazandiki na wafitini" kwa madai kuwa wamekuwa hawawaelezi wanachama wao kuhusu maendeleo ya mazungumzo baina ya pande hizo.

Katika hotuba hiyo ya dakika 95, ambayo pia ilirushwa moja kwa moja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), TBC Taifa na redio Uhuru, Rais Kikwete, ambaye alikuwa akishangiliwa mara kwa mara na wazee hao ambao wengi walivalia mavazi ya rangi za njano na kijani, alitangaza mgomo huo kuwa ni batili kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.

Bi Asha, ambaye ni mkulima wa jembe la mkono, alisema rais hakutumia hekima na busara katika kutatua kero za wafanyakazi bali alitumia cheo chake kuwatisha wafanyakazi katika kutetea haki zao.

Alisema kwamba serikali inapaswa kuweka umuhimu wa kutatua kero za wafanyakazi kwa kuwa ndio wanaotoa huduma zote muhimu kwa wananchi wote hasa masikini ambao ni wakulima.

Alisema rais na familia yake wanatibiwa nje ya nchi ndiyo mana haoni umuhimu wa kutatua kero za wafanyakazi badala yake anatoa majibu ya dharau kuwa kama hawataki kufanya kazi waache.

“Au kwa kuwa rais na viongozi wenzake wanatibiwa Ulaya na Marekani ndio maana anatoa vitisho au anataka uwe kama mgomo wa mwaka juzi kwenye Hospitali (ya Taifa) ya Muhimbili ambako watu walipoteza maisha,” alihoji Asha.

“Kama wafanyakazi nao wakisema liwalo na liwe wakachukua hasira kama alizochukuwa rais, itakuwaje; madaktari, manesi na watumishi wengine wakigoma, je haitasababisha maafa kwa Watanzania?”

Asha ambaye alitumia muda wa dakika 70 kueleza masikitiko yake, alisema wakati rais anawatisha wafanyakazi ili wasigome, anapaswa kufunga safari kwenda maeneo ya vjijini kujionea hiyo misaada ya matrekta na ‘Power Tiller’ kama imewafikia wananchi au inatumiwa na viongozi wa vijiji kwa maslahi yao.

Rais katika hotuba yake alisema serikali haiwezi kulipa kima cha chini cha Sh315,000 kwa watumishi wa umma kwa sababu wananchi wengine watakosa huduma za afya, pembejeo za kilimo na hata vifaa vya elimu na walimu.

“Sisi wakulima hatuwezi kugoma lakini kwa muda mrefu hata hizo pembejeo na matrekta anayoyazungumzia hatuyaoni, mbona hachukui hatua na kutoa hotuba kali kwa maafisa wake ili na sisi tupate hizo pembejeo,” alihoji Asha ambaye ni mtoto pekee katika familia yao.

“Sisi vijijini hatuna huduma bora za afya, maji, barabara, shule na rais anasikia kila siku Watanzania wakilalamikia hali hiyo. Je kwa nini rais asitumie cheo chake kuchukua hatua kutatua matatizo ya wananchi kama alivyoamua kwa wafanyakazi,” alisema Asha kwa hasira.

Akizungumzia kupanda kwa gharama za maisha, Asha alisema enzi za utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, bei za vyakula zilikuwa zinafanana katika maduka yote, lakini sasa kila mfanyabiashara ana bei zake.

“Je serikali inashindwa kusimamia tatizo la kupanda kwa gharama za maisha au rais anawaogopa wafanyabiashara... na kama anawaogopa itakuwaje kwa Watanzania,” alihoji Asha.“Namuomba rais siku moja angalau afanye ziara ya kupita katika maduka na kuhoji au kuangalia bei za vyakula halafu alinganishe na vipato vyetu sisi Watanzania kama tunamudu.”

Katika harakati za kutatua tatizo la ugumu wa maisha yake, bibi huyo alisema alishaenda ikulu mara mbili na kugonga hodi ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), inayoongozwa na mke wa rais, Mama Salma Kikwete ili kuomba mkopo kwa ajili ya kufanya biashara.Asha alisimulia kuwa alifanikiwa kuonana na mmoja wa watendaji wa Wama na kumuelea shida yake, lakini alijibiwa kwamba fedha za Wama zina mlolongo mrefu na kwamba yeye hawezi kuzipata.

“Nilipohoji ni mlolongo gani, hakunifafanulia ila aliishia kuniambia tu kwamba ni mkubwa na huwezi kupata fedha hizi... rudi nyumbani. Nikamuuliza je hizo fedha mnazotangaza kwamba mnawakopesha wanawake ni wanawake wote au mna wanawake maalum ambao wanastahiki, sikupata jibu,” alisema Asha huku akionekana kuwa na hasira.

Baada ya hapo nilijua kuwa fedha za Wama ni za watu maalum na sio kila mwanamke.

Hata hivyo, Asha alimuomba Mwenyezi Mungu ampe amuweke katika afya njema Rais Kikwete ili aweze kutumia hekima na busara katika uongozi wake; amuepushe na kutumia ubabe na cheo chake katika kuwaongoza Watanzania.

“Uongozi ni dhamana aliyopewa na Mwenyezi Mungu na Mwenyezi: Mungu pia ndiye anayeweza kumnyang’anya dhamana hiyo wala si Watanzania kama anavyodhani, hivyo ajitahidi kuwa mwadilifu, mwenye hekima, busara na imani katika uongozi wake,” alisema Asha.Pia aliwaombea wafanyakazi ambao wanataka kuingia katika mgomo kutofanya hivyo kwa kuwa wakifanya hivyo watadhulumu haki za Watanzania.

“Nawaombea kwa Mungu viongozi wa Tucta wawashawishi wafanyakazi wasigome ili wasibebe dhima ya kudhulumu haki za Watanzania watakaokosa huduma mbalimbali kwa muda wote watakaogoma, Aaaammmiiin,” alisema Asha ambaye ni mkulima wa kilimo cha jembe la mkono.

source: Mwananchi

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...