February 16, 2009
"SIMU POCHI" NA ZAIN au ZAP
LILIYEYUKAJE HILI DUBWANA??????????
Tutafakali. Wadau niliposikia kuibwa/kutoweka au kuyeyuka kama barafu au mafuta kikaangoni isia zangu zilinituma kuwa hako kajifaa katakuwa ni kadogo tu pengine ukubwa wa simu ya kiganjani labda, haikunijia akili kuwa ni lidubwana likubwa kiasi hicho (yaani hiyo hizo kama screen mbili za kompyuta nyeupe na nyeusi mara mbili) ukweli sikuamini macho yangu nilivyonyeshwa na wahusika kuwa zilizoibwa ni kama hizi hapa!!!!!!!!!!
Cha kushangaza zaidi ni kuwa aina hii ya mashine kwa Afrika Mashariki na kati ni Tanzania tu ndo tunayo na huu ulikuwa ni msaaada wa shirika la nguvu za atomic la dunia na ilizinduliwa na JK Mwaka jana Mei tu, yaani hata mwaka mmoja bado toka tusaidiwe mashine hii.
Sitaki kutia chumvi wala kumnyooshea mtu kidole kwani polisi inaendelea na uchunguzi wake na sijui lini watamaliza, lakini nna maswali machache wadau ambayo naomba tushauriane kwa wema tu,
1. Mijidubwana mikubwa kama hii inawezawezaje kuyeyuka ka barafu hapo mezani pasi kuonekana na awaye yeyote????
2. Ikiwa ni Tz tu tunayo na tena hapo tu ORCI katika EAC and C, je yu wapi mteja au mseti ilikopelekwa hiyo mimashine? au inamatumizi gani mengine mbali na kutibu saratani??????
3. Hivi awaye yote alokuja chukua na kutoweka na mashine za namna hiyo au ukubwa huo alizibebabebaje? kwa lambo?? au katia mfukoni tu??????
4. Utaifa uko wapi kwa Watanzania wa leo jamani????? unapoiba kifaa kinachookoa maisha ya nduguzo, rafikizo, kaka na dadazo au mama na baba yako je uitwe nani????????? muuaji????? sijui ila yupo ajuaye.
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
Shibe inapoua kuliko njaa Obesity kills more people than hunger Most of the world's populations live in countries where overweight a...
-
LONDON (Dow Jones)--U.K. defense giant BAE Systems PLC (BA.LN) Tuesday was fined GBP500,000 for improper accounting in relation to the award...
-
On Tuesday, 7th July we witnessed the peak of the Saba Saba festivities. I never go to the Dar es Salaam International Trade Fair, these day...
-
HII NI HOSTEL YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI WANAPOISHI WATAALAMU WETU WA AFYA WA KESHO.
-
The Himba are an ethnic group of about 20,000 to 50,000 people living in northern Namibia, in the Kunene region (formerly K...
-
WADAU NADHANI SI VIBAYA SIKU MOJA MOJA TUKAPANUA MAWAZO KIDOGO NDO NAMNA YA KUELIMISHANA KUPITIA NJIA HII. HIKI ni kijiji kipo hapa bo...