June 3, 2009
JK kuzindua rasmi Mv Magogoni
Kamati ya Bunge yaonya ajali ya Mwakyembe
KAMATI ya Bunge ya Ulinzi na Usalama imeeleza kutofurahishwa na kauli tata zinazotolewa kuhusu ajali ya gari aliyopata mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, ikisema zinaweza kuvuruga amani na utulivu wa nchi.
Onyo hilo lilitolewa wakati kamati hiyo ikipokea taarifa ya matukio ya ajali mbalimbali nchini, ikiwemo ya mbunge huyo liyotokea mkoani Iringa wakati akisafiri kutoka Mbeya kuja Dar es salaam katikati ya mwezi uliopita.
Tahadhari hiyo ya kamati ya bunge imekuja wakati tayari kumekuwepo na mvutano kuhusu mazingira halisi ya ajali hiyo iliyotokea Makambako, Iringa.
Mkanganyiko uliopo hadi sasa ni kuhusu kauli mbili tofauti za Jeshi la Polisi, moja ikiwa imetolewa katika ripoti ya matokeo ya uchunguzi na nyingine ikisema ripoti halisi haijatoka, huku maelezo ya ajali hiyo yaliyotolewa na polisi yakitofautiana na ya Dk Mwakyembe.
Akizungumzia mkanganyiko huo jijini Dar es Salaam jana, mwenyekiti wa kamati hiyo, Wilson Masilingi, ambaye ni mbunge wa Muleba Kusini kwa tiketi ya CCM, alisema taarifa waliyopokea kutoka polisi inaonyesha ajali hiyo ni ya kawaida kama zilivyo nyingine.
"Tumepokea taarifa ya matukio ya ajali nchini, ikiwemo zinazohusiana na baadhi yetu sisi wabunge. Kuna hii ya Dk Mwakyembe ambayo polisi wanasema ni ya kawaida kama ajali nyingine tu," alisema Masilingi.
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Nimekuta ubishi paala fulani tena kwa watu naweza sema ni waelewa kiasi fulani maana wameenda shule na wengine wako katika fani, ati ile ho...
-
Prof Aloysius Mwessa Hnonoli ni Mbongo wa kwanza kuwa Mkurugenzi wa Muhimbili na Mkuu wa Chuo kikuu cha Tiba. Mstaafu huyu jana alitu...
-
WADAU NADHANI SI VIBAYA SIKU MOJA MOJA TUKAPANUA MAWAZO KIDOGO NDO NAMNA YA KUELIMISHANA KUPITIA NJIA HII. HIKI ni kijiji kipo hapa bo...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
Mgonjwa wa saratani akipata huduma Ocean Road Cancer Insititute (ORCI) asubuhi leo hii baada ya kununuliwa kwa vifaa vilivyokuwa vimeibwa y...
-
Shibe inapoua kuliko njaa Obesity kills more people than hunger Most of the world's populations live in countries where overweight a...
-
Dr H Mwakyembe akishushwa toka ktk ndege ya kukodi na kupelekwa moja kwa moja MOI kwa Matibabu zaidi, Dr Mwakyembe alipata ajali ya gari m...
-
Mineral occurrence in Tanzania by TMAA UONGEZAJI WA PATO LA MTANZANIA Mheshimiwa Spika, 46. Lengo la Dir...
-
Ukumbi huko nyuma ya Minara miwili ukiwa ni wa mviringo. Eneoe kubwa la chai na ukaguzi pamoja na usajili kwa waalikwa. Sehemu za waa...