Kijana (bila shaka shabiki wa CHADEMA) akimsadia mwenzie wa CCM kutundika bendera wakati wa kampeni zilizoisha jana huko Igunga. Picha hii nimeipata JF, nimeipenda sana, inasema maneno zaida ya 1000 kuhusu siasa jimboni humo.
Kila mtu anaweza kuwa na tafsiri yake, na hakika kila mtu ana haki kuwa na maoni au tafsiri yake, ndio demokrasia.
October 2, 2011
Igunga UPDATES: Marehemu wafufuka kupiga kura!
Kwa mujibu wa ITV Igunga Live,
- kuna wafu wamefufuka na kwenda kupiga kura leo hii,
- Watu kadhaa hawaoni majina yao vituoni
- Wapo waliopiga kura mwaka jana leo hii kadi na majina haviendani.
- Kuna baadhi vituo vifaa havijafika,
- Sehemu nyingine vimepelekwa kwa baiskeli na punda kutokana na ubovu wa miundombinu.
- Vijana wamejitokeza kwa wingi kuliko mwaka jana,
- Hari ni shwari mpaka sasa.
Wana igunga kukata mzizi wa fitina leo.
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akimnadi Mgombea wa CCM Peter Kafumu. |
Umati mkubwa wa watu ukimsikiliza Benjamin Mkapa Rais Mstaafu wa Tanzania na Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM wakati akifunga kampeni. |
Baada ya kampeni za takriban mwezi Mmoja zilizokuwa zimejaa
kila aina ya vibweka na vituko na matukio yasiyotarajiwa ambazo hazikuwai
kushuhudiwa jimboni humo na kuitimishwa kwa mbwembwe za kutimuliwa vumbi la
kutosha kutoka kwa helikopta zipatazo nne hatimaye leo hii wana Igunga wataamua
ni nani kati ya wagombea nane atakuwa mwakilishi wao.
Jumla ya
vyama nane vimesimamisha wagimbea navyo ni
- CCM Peter Kafumu
- CHADEMA – Joseph Kashindye
- CUF – Leopold Mahona
- AFP – Steven Makingi
- CHAUSTA – Hassan Ramadhani
- DP – Abdalah Chem
- UPDP – Hemed Ramadhan
- SAU – John Magifi
Kampeni za
Igunga zimeshuhudia vyama vyenye nguvu ama jeuri ya pesa vikitumia kila aina ya
usafiri na tambo kuwafikia wapiga kura kuanzia Mashangingi mpaka Helikopta huku
vinyonge vikiishia kutumia Punda na pikipiki na hivyo kuwafikia wapigakura
wachache sana achilia mbali vingine kuanza kampeni siku nne kabla ya uchaguzi.
Kila le
kheri wana Igunga.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Nimekuta ubishi paala fulani tena kwa watu naweza sema ni waelewa kiasi fulani maana wameenda shule na wengine wako katika fani, ati ile ho...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
Mgonjwa wa saratani akipata huduma Ocean Road Cancer Insititute (ORCI) asubuhi leo hii baada ya kununuliwa kwa vifaa vilivyokuwa vimeibwa y...
-
WADAU NADHANI SI VIBAYA SIKU MOJA MOJA TUKAPANUA MAWAZO KIDOGO NDO NAMNA YA KUELIMISHANA KUPITIA NJIA HII. HIKI ni kijiji kipo hapa bo...
-
Shibe inapoua kuliko njaa Obesity kills more people than hunger Most of the world's populations live in countries where overweight a...
-
HIGH COMMISSION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA Telephone:012- 342 4371/93 Fax: 012 – 430 43 83 E-mail: t anzania@cis.co.za ...
-
On Tuesday, 7th July we witnessed the peak of the Saba Saba festivities. I never go to the Dar es Salaam International Trade Fair, these day...
-
LONDON (Dow Jones)--U.K. defense giant BAE Systems PLC (BA.LN) Tuesday was fined GBP500,000 for improper accounting in relation to the award...