July 31, 2008
DEUS MALYA - ALIYEKUWA NA WANGWE
SEHEMU YA WARAKA WA CHADEMA KWA IGP MWEMA.
Hivyo basi , Chadema kama Chama kilichoathirika kwa kumpoteza Mbunge wake, Mwenyekiti wake wa Mkoa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti na hivyo kuwa na maslahi ya karibu sana katika uchunguzi huu, tunalitaka Jeshi la Polisi wakishirikiana na vyombo vingine vya Usalama kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na mambo yafuatayo;
1. Kujua huyu ambaye alikuwa (Deus Mallya) na Marehemu kwenye gari lake wakati anafariki ni nani na anafanya shughuli gani.
2. Deus Mallya alienda Dodoma kufanya shughuli gani na ana uhusiano gani na Marehemu na au Familia ya Marehemu.
3. Ndugu Deus Mallya alikuwa amekaa kwenye kiti gani wakati ajali inatokea.
4. Ni nani alikuwa anaendesha Gari wakati ajali na hatimaye umauti unamkuta Mheshimiwa Chacha Wangwe.
5. Ni mazingira gani yaliyopelekea na au kusababisha ajali hiyo kutokea .
6. Tunataka Polisi wachukue hatua stahiki za kisheria ili Deus Mallya akaisaidie Polisi na kuhojiwa kwa kina juu ya suala hili kwani maelezo yake yana utata mkubwa sana.
7. Jeshi la polisi liitoe ripoti ya uchunguzi huo mapema na kuiweka ripoti hiyo hadharani.
Tunapendekeza hatua hizo zichukuliwe mara moja kwani tunaamini kuwa kifo hiki kimeghubikwa na utata mkubwa sana na haswa kutokana na maelezo ambayo yamekuwa yakitolewa na aliyeshuhudia ajali (Deus Mallya) pamoja na watoto wa marehemu.
WANGWE - MAZISHI YAHAIRISHWA
MAZISHI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA TARIME CHACHA WANGWE YAMEHAIRISHWA KUSUBIRI UCHUNGUZI WA MAITI,
KAKA YAKE MAREHEMU PROF SAMWEL WANGWE AMENUKULIWA AKISEMA KUWA NDUGU WAMEFIKIA UAMUZI WA KUTOZIKA MWILI HUO KUTOKANA NA UTATA WA JINSI AJARI HIYO ILIVYOTOKEA, MAELEZO YA ALIYEKUWA NA MAREHEMU BW DEUS MALLYA PAMOJA NA TAARIFA ZA VYOMBO VYA HABARI VILIVYO NUKUU SHUHUDA WA KWANZA WA AJILI HIYO ENEO LA PANDAMBILI DODOMA.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
Shibe inapoua kuliko njaa Obesity kills more people than hunger Most of the world's populations live in countries where overweight a...
-
LONDON (Dow Jones)--U.K. defense giant BAE Systems PLC (BA.LN) Tuesday was fined GBP500,000 for improper accounting in relation to the award...
-
A very rare opportunity. With Outstanding Entrepreneur, Great Visionary, Motivational Speaker, Founder, Chairman and CEO of Edmark Inte...
-
On Tuesday, 7th July we witnessed the peak of the Saba Saba festivities. I never go to the Dar es Salaam International Trade Fair, these day...
-
SAKATA LA RADAR BADO BICHI KABISA......... BAE in spotlight over Tanzania radar deal BAE Systems faces fresh controversy over foreign ar...
-
HII NI HOSTEL YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI WANAPOISHI WATAALAMU WETU WA AFYA WA KESHO.