WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesikitishwa na maisha wanayoishi wanafunzi wa Shule ya Msingi Mulusagamba iloyopo wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera.
Pinda alionyesha masikitiko hayo jana baada ya kufika shuleni hapo na kuwaona wanafunzi wa shule hiyo wakitembea bila viatu huku sare zao za shule zikiwa chafu.
Waziri Mkuu huyo ambaye yuko katika ziara ya kiserikali katika Mkoa wa Kagera, alifika katika shule hiyo kwa ajili ya kupokea taarifa ya maendeleo ya Wilaya ya Ngara iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Salumu Nyakonji.
”Hali walionayo wanafunzi hawa ni mbaya sana kwani inaonekana kuchangiwa na umaskini unaowakabili wazazi wao.
“Ili kuondokana na hali hii lazima sasa viongozi wa wilaya muwe wabunifu, mbuni fursa mbalimbali zitakazowaongezea wananchi wastani wa kipato chao.
“Viongozi lazima mhakikishe wananchi wanaboresha kilimo ili kiwe na tija kwani kwa kufanya hivyo wataweza kukabiliana na umaskini wa kipato unaowakabili,” Alisema Pinda
Ili kuimarisha Kilimo Kwanza, aliwataka viongozi wilayani hapa wawahamasishe wananachi juu na manufaa ya kilimo cha kisasa kwa kufuata kanuni za kilimo.
March 10, 2011
Pinda ashangaa wanafunzi kukosa viatu.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
Shibe inapoua kuliko njaa Obesity kills more people than hunger Most of the world's populations live in countries where overweight a...
-
LONDON (Dow Jones)--U.K. defense giant BAE Systems PLC (BA.LN) Tuesday was fined GBP500,000 for improper accounting in relation to the award...
-
It’s not important to hold all the good cards in life. It`s important how well you play the cards which you hold. Often, when we lose...
-
A very rare opportunity. With Outstanding Entrepreneur, Great Visionary, Motivational Speaker, Founder, Chairman and CEO of Edmark Inte...
-
On Tuesday, 7th July we witnessed the peak of the Saba Saba festivities. I never go to the Dar es Salaam International Trade Fair, these day...
-
SAKATA LA RADAR BADO BICHI KABISA......... BAE in spotlight over Tanzania radar deal BAE Systems faces fresh controversy over foreign ar...