January 31, 2009

Blog yafungwa!!!!!!!!!!!

"MASIHI SAUDI" au www.christforsaudi.blospot.com yafungwa kwa kuhubiri kweli

Habari hii inasikitisha sana, ya mtu kukamatwa, kufungiwa gazeti tando lako ambalo umekuwa ukilitumia kuwasiliana jamii, kufikisha ujumbe na kuelezea kile unadhani ni ukweli na kukabiliwa na kesi pengine kuadhibiwa kifo kwa kueleza hisia zako tu? Huyu bwana Hamoud Bin Saleh hatakuwa wa kwanza "KUIJUA KWELI" bali yawezekana kosa lake ni kutaka na wengine hasa nduguze wa Saudi waijue kweli hii pitia blog yake ya www.christforsaudi.blogspot.com ndilo limekuwa kosa. Wale tunaoperuzi vitabu vitakatifu kuna kimoja kinasema na nanukuu " NA WATAIJUA KWELI NA HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU" swali je kweli ni ipi? Mwalimu Nyerere alipata kusema kuwa hakuna vita ya kijinga kabisa kama vita ya kidini, kwasababu dini ni imani ambayo kwanza hukuzaliwa nayo na waweza kubadili kadiri ama kuama moja kwenda ingine wakti wowote kadri uonavyo yafaa au ushawishi wake, lakini si kabila kwani kama we ni mgogo, mhaya, mhehe NK hata ufanyeje uwezi kubadili hilo. WANABLOG MWASEMAJE KUHUSU HATUA HII YA SERIKALI YA SAUDI?

JE DUNIA HII TULIONAYO YA SAYANSI NA TEKELINALOTUJIA SHERIA KANDAMIZI KAMA HIZI ZINA NAFASI GANI BADO KATIKA DUNIA KIJIJI YETU HII?

Masikini GTV!!!

Kwa wale wateja wa tv hii na hasa wapenzi wa soka habari hii si njema hata kidogo.

A company which broadcasts English Premier League football to tens of thousands of subscribers across Africa has gone into liquidation.

Gateway Broadcast Services supplied programmes under the GTV banner to countries from Kenya to Botswana.

As well as the premiership, GTV backed several domestic leagues, including Ghana, Tanzania and Uganda. The company blamed "the current financial and global crisis" for the move. This had "severely interrupted the company's abilities to secure further funding", it said in a statement.

Television services have been stopped - with subscribers receiving a short message telling them the channel is off the air. The company said it had invested $200 million in the business but that "the economic crisis...has caused excessive demands on the business."

Several African football federations and leagues will feel the effects of this sudden move.

source: bbc

IMEKAAJE HII WADAU?

Duka la vito pale J'burg linauza tanzanite ambayo yapatika Tanzania pekee, sijui kama twaitangaza vyema hichi kito cha thamani ulimwenguni kama chapatikana Bongo tu, nasema sijui kwa kuwa tunako hako kaugonjwa kaudhaifu na kutaka kila kitu wawekezaji wafanye kana kwamba liinchi hili la neema tele halina watu wake wakufiki na kufanza kwa manufaa yetu.

Hata hivyo huyu bwana katusaidia kidogo anasema "TANZANITE ONLY IN AFRICA" sasa hapa sijui kama katusaidia ama kajihelp mwenyewe maana nasikia zamani ilikuwape "S" kabla ya africa, lakini je hii yatosha?

January 30, 2009

BREAKING NEEEEEWS... MGONJA AFARIKI

CHEDIEL MGONJA ALIYEWAI KUWA WAZIRI KATIKA SERIKALI YA AWAMU YA KWANZA AMEFARIKI DUNIA LEO HII MUDA WA SAA KUMI NA MOJA JIONI KULINGANA NA TAARIFA ZILIZOTUFIKIA MUDA SI MREFU.

AJARI ZAZIDI KUTUMALIZA BONGO.

Leo hii alfajili.
WATU 15 wamefariki dunia kutokana na ajali ya magari na gari moshi zilizotokea alfajiri ya kuamkia jana katika mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro, huku zikiacha majeruhi zaidi ya 20.
Mkoani Dar es Salaam, watu tisa walikufa papo hapo na wengine 10 kujeruhiwa katika eneo la Jet Club Kipawa katika Barabara ya Nyerere wakati mkoani Morogoro, watu sita wamekufa papo hapo na wengine 10 kujeruhiwa katika ajali ya gari moshi mali ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) iliyotokea katika maeneo ya Stesheni ya Mzaganza na Kidete katika Wilaya ya Kilosa.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema ajali ya Kipawa ilitokea saa 10 alfajiri ambako gari lenye namba za usajili T700 AFT aina ya Toyota Hiace ‘Kipanya’ lililokuwa likitokea Airport kwenda Tazara, liligonga gari lenye namba za usajili T452 ACP aina ya Scania lililokuwa limeanguka katikati ya barabara na kusababisha kifo cha abiria tisa papo hapo.
Aliwataja baadhi ya waliokufa kuwa ni Ally Issa (37); Michael Maujiro; Augustino Yohana; Elly Athumani; Alfonsi Golesh; Machel Msagira (33); na John Steven.
Alisema maiti zote zimehifadhiwa katika Hospitali ya Amana wakati majeruhi 10 wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Alisema chanzo cha ajali hiyo, Kova alisema ni mwendo kasi wa dereva wa Hiace ambayo ilikuwa imebeba abiria ikitokea Machinjioni Pugu. Alidai imebainika gari hilo lilikuwa linafanya kazi usiku tu kutokana na muda wa leseni yake kumalizika.
Naye Ofisa Habari Msaidizi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Mary Ochieng, alisema hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri kiasi.
“Tunaendelea kuwapa matibabu…mmoja bado yupo ICU (chumba cha uangalizi maalumu) na tayari tumeshawaruhusu wawili,” alisema Ochieng jana mchana.
Waliolazwa ni Simon Silvesta (27); Eva Joseph (28); Karunde Osambi (32); Zamoyoni Mongera (36); Joshua Jumanne (29), Alex Msuya (65); Emilly Steven (40); Ratibu Abdallah (21).
Katika ajali ya Morogoro, ilitokea saa saba usiku wa kuamkia jana ikihusisha gari moshi lenye namba 8828 likiendeshwa na Richard Mkude (38) kwa kushirikiana na Msaidizi wake Lucas Isaya, wote ni wakazi wa Mkoa wa Morogoro.
Gari moshi hiyo iliyokuwa na mabehewa manne, ilikuwa ikitokea mikoa ya Bara kwenda Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Reli, Yessaya Msigwa, alithibitisha ajali hiyo na akizungumza kwa simu akiwa eneo la tukio, alisema katika mabehewa hayo manne, moja lilikuwa la abiria, jingine lilikuwa tupu wakati jingine lilibeba mataluma yakitokea Wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa.
Alisema gari moshi hilo lilipofika Kijiji cha Msaganza, behewa la moja la nyuma liliyumba na kufuatia behewa lililowabeba abiria na baadaye yote kupinduka na kusababisha vifo vya watu hao na majeruhi hao walikuwa wakitoka mnadani.
Kamanda Msigwa aliwataja waliokufa katika ajali hiyo ni wafanyabiashara Said Pindupindu, Seif Bakari, Nassoro Mohamed, Jonas Lukanda, Abbas Kandaro; wote kutoka Wilaya ya Kilosa na mwingine mmoja ambaye jina lake halijatambuliwa.
Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa ni Hamisi Chamwitu; Seleman Mohamed, Sadic Monera, Esta Mbwambo na Asha Hamis ambao ni wakazi wa Mkoa wa Morogoro.
Wengine waliolazwa katika hospitali hiyo ni Edward Athanas, Aziz Seleman ambao ni wakazi wa Dar es Salaam; Hamis Manyeleta, Hamis Selemani, Mecha Jackson ambao ni wakazi wa Wilaya ya Kilosa.
Kamanda huyo alisema miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.
Alisema kazi ya kutambua miili hiyo ikikuwa ikiendelea na hadi kufikia jana mchana, miili ya watu watano kati ya sita ilikuwa imeshatambuliwa na ndugu zao na majeruhi wanaendelea vizuri.

Kilio cha Mtu mzima.......

Ukiona mtu mzima analia basi ujue kuna makubwa yamemkuta, hapana shaka aliyokutana nayo au kuyasikia toka kwa waathirika wenyewe yaani Maalbino maalufu kama "kinywa cha farasi" alishindwa kuzuia chozi lake akifafanua kwa waheshimiwa hasa waliomshutuma kuwa alikuwa ameenda kinyume na katiba.

Akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, ambaye ni Mbunge wa Wawi (CUF), kwa uchungu, Pinda alisema kauli aliyoitumia ni katika kuwahakikishia wauaji hao kuwa Serikali sasa imechoshwa na unyama wanaoufanya na wasidhani Taifa na Watanzania watawavumilia.

“Pengine kuna mtu ambaye hajapata nafasi ya kuonana ana kwa ana na kuzungumza na watu hawa (albino), mimi nimekutana nao nimeona jinsi wanavyoumia (analia), mimi nilisema kuwa wauaji hawa hawawezi kuvumiliwa,” alisema Waziri Mkuu huyo na kukatisha kidogo hotuba yake na kulia.

Huku akifuta machozi, aliendelea kusema iwapo kuna Mtanzania ambaye anaona kuwa ametenda uovu kuliko maovu yote katika suala hilo la albino na iwe hivyo, lakini nia yake ilikuwa nzuri. Alisema alianza ziara yake katika Mkoa wa Tabora, baada ya kupewa kiundani historia ya mauaji hayo ambayo yalianzia kwa vikongwe ambao kwa takwimu alizopewa, waliouawa kwa mapanga walifikia 2,000 kwa sababu za kishirikina.

Alisema wakati mauaji hayo yakiendelea kukemewa, mwaka 2006 yalianza mauaji ya albino kwa kasi ndogo, lakini hadi juzi akiwa katika ziara hiyo, alipewa takwimu kuwa walifikia 28 na wengine watatu wakauawa akiwa bado katika ziara hiyo.

Aliongeza kuwa kwa watu ambao wameyashuhudia mauaji hayo, si mazuri na ni ya kutisha kwa kuwa wauaji wanachotaka ni viungo. “Tukio la Januari 22 wenyewe mliona yule baba wa watu alipokatwa mguu wa kulia na kisha kutelekezwa hapo, damu ilimwagika hadi akafa.” Alisema pamoja na Tanzania kusifika ndani na nje ya nchi kuwa ni nchi yenye amani na utulivu, mauaji hayo sasa yameitia doa nchi.

“Kutokana na mazingira haya, niliamua kufanya ziara na katika ziara yangu nilisisitiza umuhimu wa vyombo vya Dola katika kudhibiti mauaji haya, elimu kusambazwa kwa wananchi, kuongezwa kwa huduma za afya, madhehebu ya dini kukemea mauaji hayo na vyama vya siasa kuungana katika kupambana na tatizo hilo,” alisema.

January 28, 2009

JK AMTEMBELEA ATHUMAN KHAMIS SAUZ

Rais Jakaya Kikwete pamoja na majukumu makubwa ya usuluhishi juu ya Zimbabwe lakini pia jana alipata nafasi ya kumjulia khari mpiganaji Athumani Khamis anayeendelea na matibabu huko Sauzi, kwa kweli khari ya mpiganaji inatia matumaini sana na twazidi kumwombea Mungu apate kupona kabisa na hili lawezekana tena sana.

January 27, 2009

Liumba na Kweka wapanda kizimbani.

Amatus Liumba Deogratius Kweka. Watuhumiwa Amatus Liumba na Deo Kweka waliokuwa watumishi wa BOT wamepandishwa kizimbani kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia hasara serikali zaidi ya Bilioni 220 TZS na ushee. Wamepelekwa rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana ikiwapo kila mmoja kuweka dhamana ya bilioni 50 TZS.

JE PICHA HUSOMAYO GAZETINI NDIVYO ILIVYOPIGWA?

Origino picha
Origno picha

Tumekuwa na ugomvi mkubwa sana na rafiki zangu watengeneza kurasa au graphic designer juu ya namna wanavyozitengeza au kuharibu katika kutengeza picha kabla ya kuchapishwa gazetini.

Hapo juu ni mifano michache tu ya jinsi gani mpiga picha waweza kuonekana bomu kwa msomaji kumbe kuna mtu mwingine ambaye hajulikani kwa msomaji ndo aliosababisha.

Mfano mmoja mdogo ni picha ya chini ofisi za ndege pale JNIA Dar, picha hii ilipigwa siku moja baada ya ATCL kuanza tene safari za ndani ya nchi huku wakiruka na abiria mmoja au wanne kwa ndege ya abiria 50, hali halisi yaonesha katika picha hii ni kwa jinsi gani pana kafoleni kadogo ktk Ofisi za PW lakini hakuna hata mmoja ATCL, lengo la picha hii ni kujaribu kuyaweka maneno au habari hii katika picha na ndivyo ilivyokabidhiwa na maelezo kama hayo.

Lakini jambo la kushangaza kesho yake picha ilitika kama ilivyo na maelezo tofauti na yale ya mpigapicha au hata habari yenyewe, jambo hili ni la kusikitisha sana, kwani mpigapicha anaonekana muongo sababu ya mtu mmoja tu.

WADAU WANA FANI MNA MAONI GANI? NITUMIE MIFANO ULIYONAYO TUIWEKE HEWANI ILI KUAMSHA MJADALA WA NINI KIFANYIKE.

January 26, 2009

Ujumbe kila kona..

Huwa nina kawaida au tabia ya kusoma kila kilichombele yangu kilichoandikwa, sijui kama kawaida/tabia hii ni mzuri au la kila mtu aweza sema lake.

Lakini jambo moja nilijualo ni kuwa kila nisomapo chochote kile sikosi kupata ujumbe au kujifunza jambo,

Ni wangapi wetu uwa twapoteza japo sekunde ka si dakika kusoma hivi vitiketi vya daladala? hebu soma kwa makini tiketi hii alafu niambie kile ulichogundua au kujifunza hapo. Jibu unalo.

Leo nimebahatika kupanda magari mawili ambalo kila moja lilikuwa na jumbe toka pande mbili za imani zetu kuu au kielelezo cha ustaarabu na utamaduni wetu watanzania wa kuweza kujichanganya pasipo kuwa na mikwaruzano na kila mtu akashika hamsini zake.

Moja wapo ni hili lililonipa tiketi hiyo, na la pili lilikuwa na kila namna ya ujumbe ndani ya basi wa Qorani takatifu kuanzia ule wa "Allah is One" N.K Lakini muziki uliokuwa ukitutumbuiza na kutusahaulisha machungu ya foleni za jiji la Bongo ulikuwa toka kwa Dada Upendo Nkone, kwa wale wapenzi wa nyimbo za Gospel mwajua ni nyimbo za aina gani dada huyu aimba au za milindimo ya namna ipi. Basi ilikuwa ni burudani kwetu sote, na hii ndio Tanzania kisiwa cha amani na ustaamilivu wa imani.

Na kwa wale wasiotaka kuokoka someni ujumbe huo.

Mpiganaji Athumani aendelea vyema.

Mpiganaji Athumani Khamis akijuliwa khari na Maofisa toka TSN, Mkumbwa Ali Naibu Mhariri Mkuu na Emmanuel Makene Katibu wa shirika katika Hospital ya Millpark huko Afrika Kusini katika jiji la Jo'burg hivi karibuni.

Khali ya Athumani inaendelea vizuri na inatia matumaini, kwani hivi sasa angalau ameanza kupata hisia miguuni na kuweza kuinua mikono ni jambo la kumshukuru Mungu sana na hakika kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu muumba wa vitu vyote nina imani kubwa kuwa siku moja Mpiganaji huyu atakuja tembea tena kwa miguu yake kwani hakuna neno gumu lakumshinda MUNGU.

Blogu hii inakuombea sana Mpiganaji upone haraka na upate kurudia maisha yako kama zamani na hali hii iwe kwako sehemu ya historia tu.

January 25, 2009

WAGANGA WA KIENYEJI WOTE WAFUTIWA LESENI...

Pinda ataka jino kwa jino Ni jinsi gani mauaji haya ya ndugu zetu hawa yanapokukele hata kufikia kiongozi kutoa amri ambayo yaweza onekana kama kuruhusu kuchukua sheria mkononi, lakini ukweli ni kuwa inakela na inasikitisha sana kuona kadri inavyopigiwa kelele na viongozi wetu ndo kama wanachochea moto vile wauaji hawa kuendelea, inatia maudhi mno.

KATIKA hali ya isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana aliwaambia wananchi kuwa wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja vikongwe ni hawana budi kuuawa kwa kuwa wakisubiri mahakama kuwahukumu, watakuwa wanakosea.

Waziri Pinda, ambaye ameanza ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kuhamasisha vita dhidi ya mauaji ya vikongwe na albino, aliutaka Umoja wa Vijana wa CCM kuongoza vita hiyo, akisema lina jeshi zuri.

Mauaji ya albino yamekuwa ni tatizo kubwa nchini na hasa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

January 23, 2009

Hii kali!! wagoni wote wangekuwa ka jamaaa huyu!!!!!!!

WANASEMA KUCHEKA KUNAONGEZA SIKU ZA KUISHI DUNIANI.........CHEKA UISHI ZAIDI......................

JE NANI ANA MOYO MGUMU KA MSHIKAJI

NYUMA YA PAZIA KUAPISHWA OBAMA

Behind the curtain. " Du siamini kama ni kweli ndo naenda kuchukua linchi, kiroho kinandunda kweli, yaani hawa jamaaaa wamekubari kweli au watanchenjia huko nje............"
"Enhe!! ebu tujaribu kwanza, we utanshikia hivi afu mi nitamwaga sera mama.."
"Wacha niweke mambo sawa,mhh! aka katai mbona ka kamanzese vile? au jamaa wamenibambika nini? ahha potelea mbali nani atajua bwana.

NYUMA YA PAZIA -SPEECH YA OBAMA

OBAMA'S SPEECH-BEHIND CURTAIN SHOTS. Hii ndo teleprompter ambapo speech inasomeka lakini walio mbele hawaoni maneno.
Obama akijadili na wahandishi wa hotuba yake na kuahariri.
Obama akipitia speech yake.

Mashitaka kitandani

Mwendesha mashitaka wa serikali Harun Matagane (kushoto) akimsomea mashitaka dereva Damian Aweda Lali (30) akiwa kitandani katika wodi ya majeruhi hospitali ya Mount Meru mjini Arusha kwa kusababisha vifo vya watu 16 na majeruhi 24.Kwa mujibu wa hati hiyo ya mashitaka dereva huyo alisomewa makosa 47 ya kuvunja sheria za usalama barabarani.Kulia kabisa (mwenye miwani) ni hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Arusha anayesikiliza kesi anayesikiliza kesi hiyo George Hubert.

January 22, 2009

Air Tanzania kurudi hewani kesho!!

Shirika la ndege la Tanzania litaanza rasmi tena kurusha ndege zake kwa safari za ndani tu kwanza.

Ubishi mwingine!!! ati OBAMA hakusoma speech yake!!!!!!

Nimekuta ubishi paala fulani tena kwa watu naweza sema ni waelewa kiasi fulani maana wameenda shule na wengine wako katika fani, ati ile hotuba aliyotoa mara baada ya kuapishwa ati hakuwa akisoma popote ila ilikuwa yatoka kichwani tu!!!

Nilishangaa sana kusikia vile, lakini nikaona si vyema nikanyamaza nikaona nililete kwenu wadau, je kuna anayehamini kuwa BO alikuwa hasomi ile speech?

Nawaombeni nitumieni maoni yenu tafadhali ili tusaidie wale wasiojua ili angalau wapate mwanga.

January 21, 2009

Ajari mbaya tena Arusha, 16 wafa papo hapo.

Ajari mbaya imetokea leo alasiri baada ya basi la abiria aina Coaster lenye namba za usajili T799 AWR kugongwa na roli la kampuni ya Bonite na kusababisha vifo vya watu wapatao 16 katika Daraja la Mto Nduruma katika barabara kuu ya Arusha-Moshi.

JK, PINDA ZIARANI NA MAUAJI YA ALBINO.

Rais JAKAYA kikwete akimsalimia mtoto yusuf sheha ambaye ni albino katika kijiji cha konde, Pemba
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika mkutano aliouitisha wa kujadili mikakati ya kukomesha mauaji ya albino na vikongwe akiwa na mototo Stella wakati alipozungumza na viongozi wa serikali, vyama vya siasa , dini na maalbino kwenye ukumbi wa Vijana katika mji Mdogo wa Chato,
Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda akiwa na mototo George Bush wa Chato ambaye Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe walimwomba kwa wazazi wake ili wakaishi naye nyumbani kwao, wakamsomeshe na kumsaidia kwa kila hadi atapojitegemea.
Waziri John Magufuli akiwa na mbunge wa Kuteuliwa Sheimaa Kwegir.

HAPANA SHAKA KUWA VIONGOZI WETU WAKO MSTARI WA MBELE KATIKA KUPIGA VITA UKATILI UNAOFANYWA KWA NDUGU ZETU HAWA. BRAVO JK, BRAVO MTOTO WA MKULIMA.

January 20, 2009

KAGODA FILES, WAMILIKI HAWA HAPA..

Wakala wa usajili wa makampuni wakanusha faili la Kagoda Agriculture Ltd kupotea, Mkurugenzi Bw Estarino Mahingila aonesha despatch kama ushaidi kuwa lilichukuliwa na PCCB kwa uchunguzi.
Pia aliwataja wamiriki kuwa ni John Kyomuendo na Fransis William.
Kampuni hii ni moja ambayo ilichota kiasi kikubwa cha pesa Billioni 40 peke yake ktk akaunti ya EPA.

UDAHILI WAENDELEA UDSM

YALIYOJILI HUKO UDSM KWA UFUPI
UDAHILI KWA WANAFUNZI WA UDSM UNAOTARAJIWA KUCHUKUA WIKI MOJA UMEINGIA SIKU YA PILI LEO, AMBAPO UONGOZI WA DARUSO UNASHIKILIA MSIMAMO KUWA WANAFUNZI WOTE WAREJESHWE LA SIVYO HAPATASOMEKA PALE NA KUWA WAKOTAYARI KUJITOA MHANGA ILI WANAFUNZI WAPATAO 2000 WALIOSHINDWA KUTIMISHA MASHARTI WANARUHUSIWA KUENDELEA NA MASOMO.

Julius Nyerere Convention Center yaja.

WACHINA KUJENGE UKUMBI KUMUENZI NYERERE
rais kikwete na balozi wa china nchini mhe.liu xinsheng wakiangalia mchoro wa jengo linalotarajiwa kujengwa jijini dar es salaam lijulikanalo kama julius nyerere convetion center wakati walipokutana ikulu

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...