March 20, 2009

Lipumba aunga mkono ununuzi wa Dowans

Prof Lipumba aungana na hoja ya Zitto.
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ametetea uamuzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutaka kununua mitambo iliyotumika ya kufua umeme.
Lipumba amesema uamuzi wa kununua ‘mitumba’ si mbaya ila cha kuzingatiwa ni kama mitambo itakayonunuliwa itakuwa na manufaa kwa nchi.
Hoja hiyo ni sawa na iliyotolewa na kusimamiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye alisema ununuzi wa mitambo ya Kampuni ya Dowans Limited, unazingatia maslahi ya Taifa, licha ya sheria ya manunuzi kuzuia.

Hizi ndo zile bike zilizojaa mitaani mwetu au???

Unclaimed bikes off to Tanzania
An African charity run by a Faughart priest got a boost last week thanks to Dundalk GardaĆ­ – and a bunch of unclaimed bikes.
Bikes, which have been sitting at the station for months, have been given to Fr Christy McElwee for his Tanzanian communitybuilding charity.
GardaĆ­ made a police property application to Dundalk District Court last week asking that the bikes be given to Fr McElwee for his charity.
The bikes will make a huge difference to the people of rural Tanzania, according to Fr McElwee, who got involved in the Rosminian Order-led charity about five years ago.
But it will take some more fundraising to get the much-needed bicycles to their final destination.

Nani anasababisha migogoro ya ardhi??

Wakazi wa Kwembe Kati wakizuia kwa shuka afisa wa upimaji ardhi kupima tena maeneo yao.
Pamoja na kuwepo askari wapatao ishirini wengine wakiwa na mitutu bado wananchi walikuwa ngangari kuakikisha kuwa hakuna upimaji wowote utakaofanyika tena pasipo kupewa somo kwanini wanapimiwa tena maeneo yao.
WAKAZI wa Kwembe Kati, Dar es Salaam wameendelea kuwazuia Maofisa Ardhi kupima viwanja katika eneo lao baada ya polisi zaidi ya 20 kutawanywa katika eneo lao ili wasimamie upimaji huo badala ya kutumia kamati ya wananchi kama walivyokubaliana.
Awali wakazi hao waliwazuia watendaji hao kupima viwanja hivyo vilivyo katika mradi wa viwanja 600 juzi kwa kile walichodai kutumia polisi kulazimisha upimaji badala ya kuishirikisha kamati ya wakazi kama ilivyokubaliwa katika kikao cha pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya, Fabian Massawe, kamati na maofisa ardhi hao hivi karibuni.
Pia wakazi hao takriban 300 waliyo katika mradi huo kupitia kamati yao ya watu 10 walikubaliana na uongozi wa wilaya kupitia upya mapendekezo ambayo yanahusu fidia kwa wale ambao miundombinu kama barabara, zinapita katika maeneo yao na wenye hati tayari baada ya kuonekana wanapata viwanja vidogo kuliko makubaliano.
“Tulipeleka mapendekezo kumi ambayo yalipaswa kutolewa majibu kabla maofisa hawa hawajaja kuendelea kupima, tulitaka ufafanuzi kuhusu ramani inayotumika na namna ambavyo mipaka ya mawe inawekwa juu ya mipaka mingine, tulitaka hayo yarekebishwe lakini tunashangaa wanakuja na polisi,” alisema Jackton Manyerere mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.
“Tunampataka Kanuti (jina la kwanza ni Dioscory Kanuti-Ofisa Mipango Ardhi) atufafanulie ramani ipi inatumika maana tangu mwanzo tupo nae katika vikao na Mkuu wa Wilaya, kwa nini anatuchanganya hivi,” alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hilda Mushi ambaye ramani ya awali ilionyesha barabara inapita katikati ya nyumba yake.
Hata hivyo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Upimaji Milki Mijini, Saimon Katambi baada ya kuangalia ramani iliyokuwa inatumika, aligundua kuwa haikuwa ramani inayopaswa kutumika na ndipo alipotoa ramani halali ambapo Ndaki alipoagiza upimaji uendelee kwa ramani sahihi.
Sakata hilo lililodumu zaidi ya saa tisa, liliishia kwa wakazi hao kuwataka maofisa ardhi kukaa pamoja na kamati, Mkuu wa Wilaya na Waziri mwenye dhamana, John Chiligati, kupitia mapendekezo ya wananchi ili upiamji uendelee.
Kwembe Kati ni eneo muhimu sana kwa siku za usoni, je kwanini???
Kama jina lilivyo Kwembe Kati, ipo katikati ya miradi miwili mikubwa sana ya siku za usoni, upande mmoja ukiwa ni eneo la wa mji mpya wa Dar au "Setilite City" ambao utajengwa hapo Kibamba na mwingine ni Chuo kikuu cha Tiba cha muhimbili ambacho nacha kipo upande wa pili wa eneo hili ivyo kwa siku za usoni hii ni kama Magomeni au Kinondoni flani ivi.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...