July 10, 2008
Rostam azua balaa
AYA NDO YALINUKULIWA NA MDAU TOKA KINYWA CHA ROSTAM AZIZ MBUNGE WA IGUNGA AMBAYO IMEKUWA GUMZO HATA KUSABABISHA KUSIMAMISHWA KWA MTUMISHI ALIYEMWALIKA MFANYABIASIASA HUYU.
Tuliombee Taifa – Rostam Aziz
Asema watu wanachukuiana na kuombeana vifo
Adai wanazushiana uchawi, anapakaziwa fisadi
Aomba kanisa litumike kurejesha taifa katika mstari
Dar es Salaam, Julai 6, 2008
MBUNGE wa Igunga, Bw. Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu kisiasa na kujamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari ulio sahihi.
Bw. Rostam alitoa mwito huo Dar es Salaam jana katika hafla ya uzinduzi na kuweka wakfu albamu ya kwaya ya Amkeni ya Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kinondoni, iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Alisema waumini wa dini hawamtuhumu mtu, hawamshutumu, hawapendi wenye wivu na wenye chuki bali wanapenda haki, na kwamba licha ya kashfa za ufisadi anazozushiwa, wamepuuza hilo na wamejenga imani kwake.
“Nawashukuru kwa kuamua kunialika kuwa mgeni rasmi… ni ishara kwamba mmeamua kupuuza maneno na upuuzi wa vijiweni. Nafurahi kuwa miongoni mwenu…. hamtuhumu, hamshutumu, hampendi wenye wivu na wenye chuki, mnapenda haki. Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii,” alisema Rostam huku akishangiliwa na umati wa watu waliofurika katika hafla hiyo.
Rostam alisema watu wanachukiana mpaka kufikia hatua ya kuzushiana uchawi na kuombeana vifo. “Tutumie makanisa kukemea vitu hivi ili kurejesha taifa katika mstari ulio sahihi,” alisema.
Rostam alisema licha ya matatizo ya kisiasa, kuna matatizo ya kijamii ambayo alisema ni ndoa kuvunjika kila kukicha, watoto wa mitaani kuongezeka, madanguro na dawa za kulevya kukithiri, mambo ambayo yanasababishwa na mmomonyoko wa maadili.
Katika hafla hiyo ya kuweka wakfu kanda za video, kaseti na dvd, Mbunge huyo alitoa mchango wa sh. milioni 5 kuchangia seti za vyombo vya muziki kwa kwaya ya Amkeni pamoja na jenereta yenye thamani ya sh. milioni 2.6. Hiyo ni albamu ya kwanza ya kwaya ya Amkeni iliyodumu kwa miaka 24 sasa.
Mwaka 2005, Rostam pia alishiriki katika harambee ya ujenzi wa jingo la Kanisa la KKKT Kinondoni ambalo kwa sasa linatumika kama Chuo Kikuu cha Tumaini.
Mwisho…
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Umati wa watu unaozidi kufurika huko Loliondo kwa dhumuni moja tu, kupata dawa ambayo inaaminika inatibu magonjwa sugu ama yaliyoshin...
-
Uongozi wa Shule za Marian Bagamoyo unawakaribisha wote kwenye Fundraising Dinner hii ili kuchangisha fedha ya Kujenga na kue...
-
August 13-16th, 2009 in Nairobi, Kenya. Kelele is an annual African bloggers’ conference held in a different African city each year and ru...
-
Mtuhumiwa namba moja wa kesi ya BOT Amatus Liyumba ameibuka leo mahakamani Kisutu kinyume na taarifa kuwa alikuwa ametoweka.
-
Our physical appearance is a reflection of our state of health. Being overweight is an indication of a highly toxic body due to poor digesti...
-
Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu, poses for a photo before dinner at Tivoli in São Paulo, Brazil on August 28, 2011. She wi...
-
Porn image ban sparks concern A new law, slated to come into force in January, will make the possession of images deemed to be of an extre...
-
This morning I heard a true and sad story from a colleague of mine. She told me one of her friends is always having miscarriages. When the b...
-
WINNERS Boulevard.: Biashara ya Masoko ya Mtandao : Fikiria kama ungekuwa walipwa kwa kila ushauri wa kutumia huduma ama bidhaa ya kampuni a...
No comments:
Post a Comment