June 18, 2008
Karibu Bongo Kelly Rowland
Bila shaka utakuwa bado unalikumbuka kundi maarufu la muziki lililokuwa linajulikana kama Destiny’s Child kutoka nchini Marekani. Miongoni mwa mabinti waliokuwa wanaunda kundi hilo ni Kelly Rowland(pichani).Wenzake walikuwa ni Beyonce Knowles(mke wa Jay Z hivi sasa) na Michelle Williams. Kundi hilo lilivunjika rasmi mwaka 2005 ingawa mara moja moja bado huwa inatokea wakafanya maonyesho pamoja.
Baada ya kuvunjika kwa kundi lao na kila mmoja kuendelea kivyake na shughuli za kimuziki,uigizaji nk, Kelly Rowland amekuwa akijitolea sana kwa huduma za kijamii.Hali hiyo ndio imemfanya achaguliwe hivi karibuni kuwa Balozi wa Taasisi ya MTV Staying Alive ambayo imejikita katika kupigana vita na maradhi ya ukimwi pamoja na matokeo yake kama vile kuwanyanyapaa walioathirika nk.
Ni katika wadhifa huo wa “ubalozi” ambapo Kelly Rowland anatarajiwa kutua nchini Tanzania hivi leo ikiwa ni katika ziara yake katika nchi kadhaa za Afrika ikiwa na nia ya kueneza ujumbe na kuendeleza kazi za taasisi hiyo.
Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania ambao ndio wenyeji wake,Kelly Rowland anatarajia kutembelea vituo kadhaa vinavyojishughulisha na mapambano dhidi ya ukimwi na pia kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara yake. Akimaliza ziara yake nchini Tanzania,Kelly Rowland anatarajiwa kuelekea Kenya na kisha Ghana,Msumbiji na Angola.
Halafu bonyeza hapa uone jinsi mwanamuziki huyu na nduguze walivyopewa heka heka na nyani katika mojawapo ya nchi za kiafrika anazozitembelea.
By BC.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576
Popular Posts
-
At least 32 people have been killed in multiple explosions after an accident at a munitions dump in Tanzania's commercial capital, Dar e...
-
KASHFA YA RICHMOND YAPELEKEA Lowassa kujiuzuru, hii ina maana gani wapendwa? je na baraza zima limepigwa chini au niaje? Pichani juu ak...
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakiangalia uandaaji wa huduma mbali...
-
Wiki moja tu baada ya serikali kutangaza kuanza kutoza ushuru kwa mashirika ya Dini wakti ikiwasilisha bajeti ya Mwaka 2009/10 Waziri Mkuu M...
-
Mgombea wa CCM Oscar Mukasa akipiga kura. Matokeo ya awali ya uchaguzi mdogo wa Biharamulo yanaonesha mchuano mkali sana kati ya CCM na CH...
-
MGOMO WANUKIA TAZARA Wafanyakazi wa TAZARA kupitia chama cha wafanyakazi wa reli leo wametangaza mgogoro na uongozi wakidai kulipwa mishahar...
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
WADAU NADHANI SI VIBAYA SIKU MOJA MOJA TUKAPANUA MAWAZO KIDOGO NDO NAMNA YA KUELIMISHANA KUPITIA NJIA HII. HIKI ni kijiji kipo hapa bo...


No comments:
Post a Comment