Yaaminika kuwa mwili uliokotwa uko Kwembe ukiwa umearibika vibaya kuwa ni wa aliyekuwa Dereva wa Naibu Waziri Usalama wa Raia aliyetoweka yapata wiki mbili sasa Bw Tumaini Mbaga,
pamoja na kuwa inasubiriwa taarifa ya mkemia mkuu, Mke wa dereva huyo ametambua baadhi ya vitu kama suruali, soksi na kitambaa kuwa ni vya mumewe,
Mpaka sasa hakuna aliyekamatwa kuhusishwa na utekaji au mauaji ya dereva huyo, na bado ni kitendawili kikubwa juu ya lengo hasa la wauaji wake hasa ikizingatiwa kuwa gari lilipatika likiwa limetelekezwa CCM Tabata siku moja tu baada ya kuchukuliwa CCM Temboni.
No comments:
Post a Comment