September 5, 2014

Lau watu wote wa BWANA wangekuwa Manabii - We need more Prophets now than before.

Nabii BG Malisa wa Ukombozi Ministry for All Nations.

Kwa mujibu wa Biblia takatifu, Mungu ameweka huduma ama karama zipatazo tano katika kanisa ili kuujenga na kuukamilisha mwili wa Kristo ambazo ni mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu. (Waefeso 4:11, 1 Wakorintho 12:28)

Huduma zote hizi ni muhimu sana kwa ustawi wa kanisa na katika kutimiza kusudi ama lengo la kuhubiri injili duniani kote na kuwafanya watu wote wawe wanafunzi wa Kristo. Hakuna iliyo kuu kuliko nyingine.


Kanisa linahitaji huduma zote hizi kwa zama na nyakati tofauti tofauti, lakini kwa nyakati tulizo nazo sasa twahitaji huduma ya kinabii zaidi, labda si ajabu kuona hivi sasa watumishi wengi wakaamua huduma au karama zao kuwa ni unabii, ni kimaandiko.

Nabii BG Malisa.

Nyakati tulizo nazo ni nyakati za uhaba wa neno la Mungu, nyakati ambapo tungependa kujua yatakayotukia kabla hayajatukia, tungependa kujua mwisho wa vifungo vyetu, mwisho wa utumwa wetu, kuzijua siri za Mungu.
   

Maandiko yanasema, “Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho.” Waefeso 3:5,  hii yaonesha kuwa zamani hizi tunahitaji Roho Mtakatifu kuwafunulia watakatifu manabii wa zama zetu.
Nabii BG Malisa katika moja ya ibada za kinabii.

Ikiwa tunataka kujua siri za ufalme wa Mungu, tunahitaji manabii wa kweli, ikiwa tunataka kuthibitika, kufanikiwa, kupona, kushinda maadui zetu tunahitaji neno la kinabii toka kwa Mungu, imeandkiwa “Mwaminini BWANA Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake ndivyo mtakavyofanikiwa.” 2 Nyakati 20:20

Katika zama zetu hizi tuna manabii wengi sana, wapo wa uongo kama vile ilivyo kwa huduma zingine na wa ukweli pia, wawezaje kuwatofautisha manabii wa ukweli na wa uongo? Biblia inasema, tutawatambua kwa matunda yao. Kutokana na matunda hayo, dunia inashuudia watu wakifunga safari toka pande za dunia kuja Tanzania kwa Nabii BG Malisa kama ilivyokuwa wakienda Nigeria kwa Nabii TB Joshua kupata ufumbuzi wa yale yanayowasibu kupitia huduma ya kinabii.

Semina ya siku nane ya kuvunja maagano iliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 17 -24 Agosti chini ya huduma ya kinabii inayoongozwa na Mtu wa Mungu Nabii BG Malisa, iliyoshuudia watu wakisafiri toka Ujerumani, Marekani, DRC Congo, Kenya n.k wakija kumtafuta Mungu Tegeta, Tanzania imedhiirisha umuhimu wa jicho la Mungu katika kanisa.   
Prophet TB Joshua

Nabii ni jicho la Mungu, ana uwezo wa kuona yale ambayo kwa jicho la kawaida uwezi kuyaona, kuiona kesho, leo, kuona mwisho wa jambo mwanzoni, sawa na neno la Mungu, katika Isaya 42:9 “Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, name nayahubiri mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake”

Katika semina hii tumeshuhudia unabii ukitolewa kwa usahihi na watu wengi walifunguliwa papo hapo kwa neno la unabii toka Mtu wa Mungu kama alivyoongozwa na Roho wa Mungu.
Lakini huduma hii, tofauti na huduma nyingine, imekuwa ikikutana na shutuma na laumu nyingi, tena nyingi ya shutuma hizo zinatoka kwa baadhi ya watumishi (Wachungaji, Mitume, Waalimu au Wainjilisti), kana kwamba hii ni huduma mpya kabisa.

Hili halishangazi sana, waliopinga huduma ya Yesu walikuwa ni wakuu wa dini (mafarisayo, makuhani na waandishi), watumishi hao wanasahau kuwa imeandikwa katika Waefeso 4:11, “ Naye alitoa wengine kuwa  mitume, na wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu”.

Tena imeandikwa, “Na Mungu ameweka wengine katika kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kasha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi ya na aina za lugha.” 1 Wakorintho 12:28
Prophet TB Joshua during service.

Kwa mujibu wa andiko hilo, huduma ya Kinabii ni ya pili baada ya ile ya kitume, kwani imeandikwa kuwa “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.” Amosi 3:7, ni wazi kuwa kanisa la Kristo linahitaji sana huduma hii sasa kuliko wakati mwingine ili Mungu aweze kufanya lolote katika maisha yetu.



Musa alikuwa nabii mkubwa sana wa Mungu, biblia inasema “wala hajainuka tena katika Israel nabii kama Musa, ambaye BWANA alimjua uso kwa uso” Kumbu 34:10, lakini Musa alitamani sana watu wote wa BWANA angewatia Roho wake wawe manabii, yaani wote waliompokea Kristo wawe manabii. (Hesabu 11:29). 

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...