September 15, 2011

Mv Spice Islanders 1 - watu 2000 hawajulikani walipo!


MELI ya MV Spice Islanders iliyopata ajali mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha vifo vya takriban watu 200 na majeruhi 619 ambao waliokopolewa, ilibeba abiria 3,000 wakati uwezo wake ni kubeba abiria 600 tu.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa idadi hiyo kubwa ya abiria, haijumuishi mizigo ambayo kiasi chake bado hakijajulikana.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Fakhi Dadi alisema jana kuwa mkoa huo umepoteza watu 1,600 katika ajali hiyo, huku Wilaya ya Wete pekee ikiwa imepoteza watu 1,141.Dadi alisema hayo alipokuwa akizungumza mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
 
“Wilaya ya Micheweni imepoteza watu 367, huku Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba ikipoteza watu 27 na Wilaya ya Chakechake imepoteza watu 148,” alisema Dadi na kuongeza:
 
“Kwa idadi hiyo ikijumlishwa na idadi ya watu 619 waliosalimika katika ajali hiyo na wengine 204 waliotambuliwa na kuzikwa na wengine watano waliookotwa Mombasa, huenda meli ile ilikuwa na watu 3, 000,” alisema Dadi.
 
Kutokana na takwimu zinazoendelea kukusanywa, hadi sasa zaidi ya watu 2,000 hawajulikani walipo, mbali ya wale 198 walioopolewa na kuzikwa na wengine 619 walionusurika….

Source: Mwananchi 

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...