Pengine ni ndoto za mchana au ni jinamizi lilinikumba nikajikuta naota eti Mahakama ya Rufaa imeuzwa na ati inatarajiwa kuvunjwa, siamini, nadhani ni ndoto za mchana tu ndo zinanisumbua, sidhani kuwa serikali yangu hii, niloichagua na kuiweka madarakani inaweza kufanya jambo kama hilo, sidhani, na haiwezekani.
Ndoto za mchana uwa ni mbaya wakati mwingine, ni rahisi kuota umeokota bulungutu na kuamka ukiwa lofa zaidi, eti ile hoteli jirani yake imeihisi inabanwa na mahakama ile na sasa inataka iondoe kiwingu, ati wageni wakiona majoho ya waheshimiwa majaji wetu wanaweweseka vyumbani, mvinyo haupandi, wanaota majinamizi! Mhh ni kweli habari hii? Mbona yule kiongozi wa taifa kubwa kabisa duniani alilala hapo siku kadhaa na hakuweweseka? ahh, ndo mambo ya ndoto hayo unakurupuka unadhani ni kweli, walinganisha na uhalisia waona kuna walakini ndo wagundua, kumbe ni ndoto tu.
Lakini mbona ndoto hii imekuwa ndefu hivi? ati kuna wataalamu fulani (si wa sheria) wanataka kuandamana kupinga kuvunjwa kwa mahakama hii? mhh yawezekana bado niko ndotoni, hivi wanasheria si ndo wangekuwa wakwanza kuandamana? sasa iweje wale, wanaitwaje vileee?? enhee, wasanifu ndo wawe na kimbelembele kuandamana??? Si mwaona mambo ya ndoto hayo, lakini kama ingekuwa ni kweli hata mimi ningewaunga mkono, ningeandamana, sijui mpaka wapi, kokote kule.
Ahh! ndo mambo ya ndoto za mchana hayo, usiombe ukaota, zinadanganya sana, hebu we fikiria serikali makini kama hii kweli yaweza kufanya uamuzi wa kijinga kama huo? hata siku moja haiwezekani, ni ndoto hizo, tena za mchana, silali tena mchana nisije jikuta naota na Ikulu nayo imeuzwa bure!
Jamani puuzieni, ni ndoto tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
TRA YA NCHI JIRANI YAPONDA PONDA MAGARI YALOSHINDWA KUKOMBOLEWA BANDARINI, MAGARI YAPATAYO 200 KUPONDWA DESEMBA HII, JE HUKU NI KUWA NA AK...
-
Tarime — FELISTA Laurent (15) had not been admitted to hospital in her life, until November 4, this year, when she was attacked by his fath...
-
Hii ni repoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Viwanda inayoonyesha jinsi wataalamu wetu wanavyokimbia nchi yao na kwenda kuta...
-
Habari wadau, Mnaweza shangaa leo kuja na uzi huu wa Saratani ya Utumbo mpana, kifupi mi si tatbibu na wala sina fani yoyote ya namna hi...
-
Wananchi wa Kijiji cha Mkunya wilayani Newala wakiwa wamebeba bango kubwa linalomuamba Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyekuwa anapita kiji...
-
WADAU NADHANI SI VIBAYA SIKU MOJA MOJA TUKAPANUA MAWAZO KIDOGO NDO NAMNA YA KUELIMISHANA KUPITIA NJIA HII. HIKI ni kijiji kipo hapa bo...
-
The Edmark Double Bonus Marketing Plan consists of both the Point Sharing System and the Block System. Thus, giving maximum benefits ...
-
WINNERS Boulevard.: Biashara ya Masoko ya Mtandao : Fikiria kama ungekuwa walipwa kwa kila ushauri wa kutumia huduma ama bidhaa ya kampuni a...

1 comment:
Tanzania kila kitu kinawezekana, ukweli ama ndoto, vyote vinawezekana tu.
Post a Comment