BAN KI MOON AMTAKIA KHERI JK KWENYE UCHAGUZI MKUU
NEW YORK-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amemtakia kampeni njema , Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na mafanikio mema katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Octoba.
Ban Ki Moon ametoa salamu hizo wakati wa Mazungumzo yake na Mwakilishi mpya wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue, mara baada ya Balozi huyo kumkabidhi hati zake za utambulisho katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu wa UN, pamoja na kumtakia kila la kheri na mafanikio Rais Kikwete, pia amempongeza Rais Kikwete na Tanzania kwa ujumla kwa kuwa nchi kiongozi na ya mfano wa kuigwa Barani Afrika katika kutekeleza na kuendeleza malengo ya Umoja wa Mataifa. Hususani amani na usalama Duniani
Aidha Ban Ki Moon, ameonyesha imani kubwa kwa mwakilishi huyo wa Tanzania huku akimpongeza kwa nafasi za ubalozi alizoshika nchini Kanada na Marekani kabla ya wadhifa wake huo mpya.
Akamtaka kuendeleza msimamo wa Tanzania wa kuwa nchi kiongozi katika Afrika na ndani ya Umoja wa Mataifa kwa kudumisha na kuendeleza malengo yenye maslahi kwa Serikali ya Tanzania, Bara la Afrika na Umoja wa Mataifa kwa ujumla.
Ban Ki Moon akatumia pia nafasi hiyo kutoa shukrani zake, kwa mtangulizi wa Balozi Sefue, Balozi Augustine Mahinga ambaye katibu Mkuu alimteua kuwa mwakilishi wake maalum huko Somalia.
Katibu Mkuu akabainisha kuwa kutokana na heshima kubwa ambayo Tanzania imejijengea ndani ya Umoja wa Mataifa, anaitegemea Tanzania katika kuwasiliana na mataifa mengine hasa yale yanayoendelea.
“Tanzania mmejijengea heshima kubwa ndani ya Umoja wa Mataifa, kwa hiyo usitegemee kuwa utakuwa unaisemea Tanzania peke yake, bali na mataifa mengine pia, na hilo ndio tegemeo langu kubwa kutoka kwako Mhe. Balozi” akasisitiza Ban Ki Moon.
Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu amemhakikishia Mwakilishi huyo wa Tanzania ushirikiano kutoka kwake yeye binafsi na sekretariati ya Umoja wa Mataifa.
Kwa upande wake, Balozi Ombeni Sefue amemwahidi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwamba atafanya juhudi zote kuendeleza maslahi ya Tanzania katika UN, kudumisha ushirikiano mzuri kati ya UN na Tanzania, na kuchangia katika kuendelelezaji wa majukumu na malengo ya Umoja wa Mataifa.
Akatumia nafasi hiyo Kumpongeza Katibu Mkuu kwa kusimamia vema utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia, huku akimwomba aendelee kuzihimiza na kuziomba nchini zenye uwezo mkubwa kiuchumi ziendelee kuzisaidia nchi zisizokuuwa na uwezo ili ziweze kutekeleza Malengo ya Maendeleo ya Millenia.
September 2, 2010
Kampeni njema JK - Ban Ki Moon
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Umati wa watu unaozidi kufurika huko Loliondo kwa dhumuni moja tu, kupata dawa ambayo inaaminika inatibu magonjwa sugu ama yaliyoshin...
-
Uongozi wa Shule za Marian Bagamoyo unawakaribisha wote kwenye Fundraising Dinner hii ili kuchangisha fedha ya Kujenga na kue...
-
August 13-16th, 2009 in Nairobi, Kenya. Kelele is an annual African bloggers’ conference held in a different African city each year and ru...
-
Mtuhumiwa namba moja wa kesi ya BOT Amatus Liyumba ameibuka leo mahakamani Kisutu kinyume na taarifa kuwa alikuwa ametoweka.
-
Our physical appearance is a reflection of our state of health. Being overweight is an indication of a highly toxic body due to poor digesti...
-
Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu, poses for a photo before dinner at Tivoli in São Paulo, Brazil on August 28, 2011. She wi...
-
Porn image ban sparks concern A new law, slated to come into force in January, will make the possession of images deemed to be of an extre...
-
This morning I heard a true and sad story from a colleague of mine. She told me one of her friends is always having miscarriages. When the b...
-
WINNERS Boulevard.: Biashara ya Masoko ya Mtandao : Fikiria kama ungekuwa walipwa kwa kila ushauri wa kutumia huduma ama bidhaa ya kampuni a...
No comments:
Post a Comment