Ni nini tofauti ya Pingamizi na Malalamiko?
Vyombo vingi vya habari jana na leo vimeripoti kitendo cha CHADEMA kupitia Kaimu katibu Mkuu John Mnyika kupeleka barua hile kuwa ni ama PINGAMIZI au MALALAMIKO (COMPLAINS).Lakini kulingana na nyaraka hizi alizoshika Bw Mnyika bila shaka ukiangalia vizuri utaona kuwa hilo si PINGAMIZI bali ni MALALAMIKO.
Wanasheria wanaweza kutusaidia hapa nguvu ya malalamiko na pingamizi, je ni nini tofauti ya vitu hivi viwili?
Kama alinikuliwa vyema Mgombea urais kupitia CHADEMA Dr Wilbroad Slaa alisema wangeweka pingamizi kwa Mgombea Urais wa CCM Jakaya Kikwete, sina hakika ni nini kimetokea badala ya pingamizi yakaja malalamiko, labda wamesoma alama za nyakati, sijui ila ni vyema wakatujulisha kwa faida ya Watanzania wote, vinginevyo watakuwa wanajichimbia kaburi wenyewe kwa kauli zao.
No comments:
Post a Comment