Pages

December 28, 2014

SHUHUDA - KUPITIA KITABU


SIRI ZA KUWA MFANYABIASHARA – USHUHUDA.
Mama huyu anamiliki duka la vifaa vya pikipiki maeneo ya Kariakoo lenye thamani ya zaidi milioni 200, biashara yake ilikuwa inafanya vizuri hapo kabla, lakini ghafla mauzo yalianza kushuka kwa kasi ya ajabu kutoka mauzo ya Mil 4 mpaka kuuza elfu 15 au 10 kwa siku.


Alichanganyikiwa, akatamani kufunga fremu na kurudisha kwa mwenye nyumba, alikata tamaa, akakaa nyumbani muda wa miezi mitatu, aliamua kufunga safari kutafuta msaada Nigeria kwa Mtu wa Mungu Nabii TB Joshua, baada ya maombezi alimshauri arudi Tanzania atapata mtumishi mwenye nguvu atakaye msaidia.
Hatimaye siku moja akiangalia kipindi cha saa ya Ukombozi kupitia Star TV alimwona Nabii BG Malisa , akaamua kufunga safari kufika kanisa la Ukombozi Tegeta, baada ya ibada alinunua kitabu hiki cha “Siri ya kuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa”  alitumia kitabu hiki na mwomgozo wa maombi.


Hivi sasa anashuhudia kuwa biashara yake imerudi kama zamani na mauzo kuongezeka kila siku,anashuhudia kuwa kitabu hiki kimekuwa msaada mkubwa sana, kwani kila akitumiapo anaona mpenyo.

PATA NAKALA YAKO FUATILIA HAPA.

No comments:

Post a Comment