Pages

November 19, 2011

NEWS ALERT: Ajari ya Basi la TAQWA na Lori la AZAM Watu zaidi ya 10 wafa papo hapo!!!!!!!!!!








Watu zaidi ya kumi wamekufa papo hapo huku wengine kedhaa wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la Taqwa lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Bujumbura kugongana uso kwa uso na lori la mizigo la Azam eneo la Lusaunga, Biharamulo.

 Bongo Pix imeshuudia miili kumi ikishushwa kutoka katika Fuso no UAM 267 N ambalo lilichukua miili hiyo eneo la tukio, Uongozi wa hospitali ulilazimika kuita watumishi wote hata wale waliokuwa mapumzikoni kuja kuokoa jahazi kwani ni wazi huduma yao ilikjuwa yahitajika katika kipindi hiki.

 Taarifa zaidi za idadi rasmi ya majeruhi, walliofariki na majina yao tutaipata baadaye baada ya kuongea na mamlaka husika, RPC na Mganga Mkuu wa Hospitali.

 Bongo Pix inawapa pole waliofikwa na msiba huu, na zaidi kuwaombea waliojeruhiwa wapate matibabu na kurejea katika shughuri zao.Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. 

No comments:

Post a Comment