Pages

November 20, 2011

UPDATES: AJALI YA TAQWA - 16 WAFARIKI PAPO HAPO

Watu 16 wamefariki papo hapo na wengine 17 kujeruhiwa baada ya basi la Taqwa No T635 AVC lililokuwa likitokea Dar kuelekea Bujumbura kugongana uso kwa uso na lori la Azam No RAB 255 W eneo la Lusaunga, Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera, 


Madereva ni miongoni mwa waliokufa, akiongoea na Bongo Pix kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Biharamulo Dr Michael Abila amethibitisha kupokea maiti 15 na majeruhi 12 huku majeruhi watano na maiti moja wakipokelewa katika Hospitali ya Ngara. 


Mongoni mwa waliofariki ni wanawake saba na wanaume 9 huku mtoto mdogo ambaye amepoteza mama yake katika ajali akijeruhiwa vibaya, pia miongoni mwa waliofariki walikuwepo watu watatu wa familia moja waliokuwa wakielekea harusini ambao miili yao ilichukuliwa jana. 


Majina ya marehemu na majeruhi yatapatikana muda si mrefu. 

No comments:

Post a Comment