Pages

September 12, 2011

Maafa zaida Afrika Mashariki - Moto wateketeza mamia Nairobi, Kenya

Wakati Zanzibar inaendesha sala maalumu kwa waathirika wa ajali ya Mv Spice Islanders ambapo watu zaidi ya 200 wamepoteza maisha na mamia hawajulikani walipo huku 620 wakiokolewa, jirani zetu Kenya nao wamepatikana na janga baya baada ya moto uliotokana na bomba la mafuta kulipuka na watu wapatao 120 kupoteza maisha. 

Hii si habari njema kwa upande huu wa Afrika Mashariki, hatuna budi kumuomba Mwenyezi Mungu atuondolee jinamizi hili. 


Zaidi ya watu mia moja wamekufa baada ya bomba la mafuta kupasuka na kulipuka katika katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, polisi wamesema.
 
Mlipuko huo umetokea katika eneo la viwandani la Lunga Lunga na askari wa zima moto walipambana na moto mkali ambao ulikuwa ukitishia makazi ya watu mjini humo.
 
Bomba hilo la mafuta limepita katika makazi ya watu wengi kwenye mitaa ya mabanda katikati ya mji wa Nairobi na Uwanja wa ndege.
 
Zaidi ya majeruhi 100 wamepelekwa hospitali, maafisa wanasema.
 
Msemaji wa magari ya huduma za dharura alisema waathirika wengi waliungua kiasi cha kutokufatambulika.
 
Taarifa zinasema mlipuko huo huenda umesababishwa na kishungi cha sigara kilichotupwa katika mtaro wa maji ambao ulikuwa ukielea mafuta.
 
Mafuta hayo yalivuja kutoka kwenye tangi moja katika ghala linalomilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Kenya, msemaji wa polisi Charles Owino ameliambia shirika la habari la Reuters.







Sources: BBC, Daily National, NTV

No comments:

Post a Comment