Pages

September 21, 2011

Hatimaye Muhubiri Gilbert Deya kurejeshwa Kenya kushtakiwa


Mhubiri ambaye aliyedai kuwa ana uwezo wa kuwatungisha mimba kina mama kimiujiza kupitia maombi atarudishwa nchini Kenya kukabiliana na mashtaka ya utekaji watoto.
 Gilbert Deya, ambaye huongoza misa katika eneo la Peckham London Kusini, amekuwa akikabiliana kisheria asirejeshwe Kenya tangu mwaka 2007, akidai kuwa hatua yeyote ile itakayochukuliwa dhidi yake itakiuka haki zake za kibinadamu.
 Kwa sasa Waziri wa Mashauri ya Ndani Theresa May ameamua mpango wa kumrejesha mhubiri huyo Kenya uendelee.
 Serikali ya Kenya inadai kuwa aliwaiba watoto watano kati ya mwaka 1999 na mwaka 2004.
 Wasiwasi ulizuka 2004 mara tu baada ya kipindi kimoja cha BBC radio 4 cha udadisi kwa Jina Face the Facts kupeperusha hewani shughuli zinazofanywa na Deya.
 Wanawake ambao hawangeweza kutunga mimba ama waliokuwa wamepita umri wa kuzaa, waumini katika kanisa lake la Peckham Kusini mwa London waliahidiwa wataweza kupata watoto kimiujiza.
 Lakini watoto hao walikuwa wanazaliwa katika zahanati bandia mjini Nairobi nchini Kenya.
 Watu hawa walikwenda Afrika na kurejea Uingereza na mtoto ambaye vyombo vya utawala viligundua hakuwa mtoto wao kupitia upimaji wa asidi nasaba.
Mbunge David Lammy
 Mke mmoja na mumewe ambao walipitia miujiza hiyo walirejea London na kwenda katika hospitali moja ya eneo la Tottenham eneo la mbunge David Lammy.
 "kilichojitokeza hapa ni kuwa kulikuwa na wizi wa watoto, ambao hukuwahusisha tu watu katika eneo langu la uwakilishi bali pia wanawake kadhaa waliokwenda Kenya na kurudi nyumbani wakidhani watoto waliorudi nao ni wao" alisema David Lammy.
 Gilbert Deya akihojiwa na Radio 4 mwaka 2004, alipoulizwa anajieleza vipi kuhusu kuwepo na tofauti kubwa kati ya asidi nasaba ya watoto na wazazi wao , alijibu " Watoto wanaozaliwa kimiujiza katika Kanisa letu wanazaliwa kwa miujiza ambayo binadamu hawezi kuitafakari"
 Mwaka 2007, Waziri wa Mashauri ya Ndani wa Uingereza wakati huo Jacqui Smith aliamua Deya arudishwe hadi Kenya.
 Deya alikataa rufaa dhidi ya uamuzi huo aliyoiwasilisha katika Mahakama kuu, rufaa hiyo haikufaulu na pia alikataliwa kuwasilisha malalamishi yake katika bunge la malodi.

Source: BBC

HUDUMA YAKE IPO HAPA 

1 comment:

  1. Anonymous7:09 PM GMT+3

    duI hiyo ni mpya, huyu anayejiita mtumishi wa mungu naonga mkono akakabiliane na mkono wa sheria kutokana na hayo makosa, amedanganya watu, na, amepotosha watu na ameshiriki kuiba watoto, wahubiri wa namna hii watazamwe kwa marefu na mapana, wanawasababishia matatizo wananchi na kupunguza uwezo wwao wa kufikir

    ReplyDelete